Nini kimewapata wasanii wetu? Hakuna wimbo mzuri kabisa kipindi hiki cha msiba. Wamezidiwa na TOT? Hakika Komba atakumbukwa

Tupo bize kusifia serikali ya awamu ya tano. Tukimalizana nayo tutarudi kwa nkapa
 
TOT wamefanya kazi nzuri,wimbo umeshiba maudhui na hata mirindimo yake iko njema!Kongole kwenu TOT
 
Hakika huo ndio wimbo bora umetulia na umetungwa vyema na kupangiliwa vizuri sana....hakika ukisikiliza unaona hawa ndio watunzi? Wako wapi wasanii wanao jigamba kuwa wao ni watunzi wazuri? Yuko wapi Mjomba mpoto?
Huo wimbo wa TOT ndo mzuri na una ujumbe hauchoshi kabisa huko TBC
 
TOT si ndo bendi la jeshi,inakwaje zinatunga nyimbo za CCM au zile za CCM ni za komba hazihusiani na TOT
TOT wamefanya kazi nzuri,wimbo umeshiba maudhui na hata mirindimo yake iko njema!Kongole kwenu TOT
 
Wabongofleva wao wanaweza kuimba nikapakie mgando, inama inama
 
ukiona hivyo jua marehemu hakuwa na msaada kwao kabisa yaani.
 
[emoji23][emoji23][emoji23] wao wamezoea mambo ya kudinyana tyuuh.
 
Wamezoea copy and paste bila kusahau kulazimisha colabo kwa nyimbo za watu zilizohit makwao
 
Kuna kwaya moja nimeona wanaimba kwa majonzi na kumshukuru marehemu Mkapa kwa kuwajengea daraja la kigamboni, mwendokasi na chuo Kikuu cha UDOM
 
wako sahihi, T.OT. ni bendi ya chama kumuimbia mkapa ni sawa, wasanii wako kibiashara, wamuimbie mkapa kwa gharama zao halafu baada ya msiba nani atasikiliza?
 
Kama mnaona hawawezi kutunga ingieni nyie studio tungeni nyimbo nzuri tumlilie mzee wetu mkapa
 
Mbona Peter Msechu kafanya kazi nzuri sana, au wewe haujafuatilia huu wimbo vema?. Mwisho japo si kwa umhimu ni kuwa kila zama na kitabu chake.
 
Shida ccm mnawatumia tu na kuwapa viposho uchwara,wapeni hela muone watatunga nyimbo hata 3000 za mkapa
 
Hakika huo ndio wimbo bora umetulia na umetungwa vyema na kupangiliwa vizuri sana....hakika ukisikiliza unaona hawa ndio watunzi? Wako wapi wasanii wanao jigamba kuwa wao ni watunzi wazuri? Yuko wapi Mjomba mpoto?
Mpotoo Tena! Wee huyo siku hizi so mpoto Tena. We mtu ameanza Hadi kuvaa viatu ataimba nn sasA
 
Tatizo la wasanii wetu ni ubanafsi, na hii yote imechagizwa na wao kujiingiza kwenye siasa kwa tamaa na umaarufu.
(Somebody at work).
Na wakibumburuka kuungana muda unawatuma mkono.
TOT ni tofauti na vikundi vya sanaa na wasanii wengine kwa kuwa hakuna mkubwa/maarufu zaidi ya mwenzake.
(Team at work).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…