Kuna sintofahamu inaendelea kuhusu Kampuni ya Mapembelo Cargo ambayo najihusisha na usafishaji wa mizigo, wamekuwa kimya sana kuhusu mizigo ya wateja wao.
Kuna Wafanyabiashara na Watu wengine ambao waliagiza mizigo kwa mambo binafsi, huu ni mwezi wa nne hawajapata mizigo yao kutoka China. Mimi nina miezi miwili nafuatilia mizigo yangu ambayo niliambiwa imeshafika tangu Oktoba 2024.
Ukiwasiliana nao wanakwambia “Wiki hii mzigo utatoka kulikuwa na changamoto Bandarini”, baada ya hapo wanapotea unaona kimya.
Hali hiyo inatuumiza sisi Wafanyabiashara, hawatupi majibu ya kueleweka na hatujui hatma ya mizigo yetu, mwisho wake mitaji inapotea kwa kuwa hakuna tunachoingiza.
Tunaomba Mamlaka husika ziingilie tujue nini kinaendeleaa. As we speak nasikia wamefilisika, sasa je, mizigo ya Wafanyabiashara inakuwaje? Si waseme ukweli kuliko kutupotezea muda.