DOKEZO Nini kinaendelea Kampuni ya Mapembelo Cargo? Tunalalamika kila siku mizigo yetu tuliyoagiza haifiki

DOKEZO Nini kinaendelea Kampuni ya Mapembelo Cargo? Tunalalamika kila siku mizigo yetu tuliyoagiza haifiki

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kuna sintofahamu inaendelea kuhusu Kampuni ya Mapembelo Cargo ambayo najihusisha na usafishaji wa mizigo, wamekuwa kimya sana kuhusu mizigo ya wateja wao.

Kuna Wafanyabiashara na Watu wengine ambao waliagiza mizigo kwa mambo binafsi, huu ni mwezi wa nne hawajapata mizigo yao kutoka China. Mimi nina miezi miwili nafuatilia mizigo yangu ambayo niliambiwa imeshafika tangu Oktoba 2024.

Ukiwasiliana nao wanakwambia “Wiki hii mzigo utatoka kulikuwa na changamoto Bandarini”, baada ya hapo wanapotea unaona kimya.

Hali hiyo inatuumiza sisi Wafanyabiashara, hawatupi majibu ya kueleweka na hatujui hatma ya mizigo yetu, mwisho wake mitaji inapotea kwa kuwa hakuna tunachoingiza.

Tunaomba Mamlaka husika ziingilie tujue nini kinaendeleaa. As we speak nasikia wamefilisika, sasa je, mizigo ya Wafanyabiashara inakuwaje? Si waseme ukweli kuliko kutupotezea muda.
Kufanya biashara na mbongo kipengele sana aisee. Yani hatuna huduma nzuri endelevu, huwa huduma nzuri ni mwanzo na baada ya hapo ama kutakuwa na shida ama customer care inaanza kuwa mbovu.
 
Nikuhakikishie tu bandarini hamna changamoto kubwa tena,angalao ndani ya siku 7 meli inashusha hivyo suala la bandarini si kweli.

Loose Cargo imekumbwa na fitna nyingi na viboko vya Customs(vilivyo halali) hivyo kampuni nyingi zinaelekea shimoni.

Ni ushauri wangu kwa wafanyabiashara ,badala ya kutumia hizi kampuni tumieni groupage.Hii inapunguza gharama na mnakuwa na taarifa sahihi za mzigo wenu.Lakini pia inapunguza gharama sana.CBM moja haitazidi usd 350.
Hii ndo inakuaje unaweza ukatoa elimu kidogo? The whole process
 
Back
Top Bottom