Halafu hili suala sijui kwanini linapotoshwa kiasi hiki!!! Hakuna Mmachinga aliyezuiwa kuuza filamu za nje! Hoja iliyopo mezani ni kwamba filamu za nje zifuate utaratibu uingiaji wake!!
Ilivyo ni kwamba, hata kama Bongo Movies nyingi ni low budget lakini majority zinatengenezwa kwa gharama isiyopungua 10 Million!!
Sasa wakati Bongo Movies wanatumia takribani 10 Million kuandaa filamu moja; wafanyabiashara wanatumia bundle ya TZS 1,500/= ku-download takribani movies 5 za nje na kisha kuzidurufu na kuzitowa kwa Wamachinga!!!
Sasa hoja ni kwamba, badala ya wafanyabiashara kufanya pirates; wawe wanaagiza hizo movies za nje kwa njia halali... walipe kodi kama wanavyofanya Bongo Movie n.k!!!
Itakuwa ni ujinga ulioota mizizi endapo mtu atashindwa kuiona hoja ya wana-Bongo Movies!! Hata kama Bongo Movies watengeneze filamu mzuri namna gani bado filamu iliyotengenezwa kwa Sh. 10 Million haiwezi kushindana na filamu iliyopatikana kwa Sh. 300 (mia tatu)!!!