Nini kinaendelea katika mitandao ya simu?

Nini kinaendelea katika mitandao ya simu?

Hiyo simu wame direct kwenda number nyingine.....ni either ndugu yako au rafik yko ali direct iyo simu yako au wale watu wanao uza line za simu mitaani


Sasa kutoa divert call piga *62#
Kama kuna number wame direct itatoka

Mitandao ya simu sio rahisi kukusikiliza wewe ni vijana tu wa mtaani wanataka kukupiga
Sidhani kama upo sahihi, call diverting ni tofauti kabisa na call interference, anacholalamika mdau ni kuwa Kuna mtu anaingilia maongezi ya simu zake na hii kimawasiliano ni kesi sio huduma.
Call diverting ni kwamba simu zako zikipigwa zinapokelewa upande wa pili bila ya wewe kujua
 
Nachojua airtel na tigo wanaya censor baadhi ya maneno kama hela na sex. Ukiyaweka kwenye msg, msg husika haimfikii unae mtumia. So kama kwako msg yenye neno hela inafika its likely airtel ndo wanafanya hiyo michezo.
Hilo la maneno linahusiana na nini mkuu,maana kweli mm mwenyewe nikiandika neno sex kwenye msg haiendi[emoji23]
 
Wana wa Jamiiforums, Nawasalimu.

Sina uhakika kama hili linatokea kwangu tu au ni kwa kila mtu zaidi ya mara tatu au nne imetokea kwamba nikipiga tu simu kwa mtu tukajadili habari ya hela ambayo pengine natakiwa kuituma kwa njia ya simu pindi nikikata tu simu meseji inaingia kuwa tuma kwa namba hii.

Leo hii saa nne na dakika 21 nimepiga simu kuuliza nauli ya basi kutoka Musoma kwenda Arusha kwa njia zote mbili kwa maana ya Musoma via Serengeti na Musoma via Singida baada tu ya kukata simu saa 10:38 meseji kaingia kwamba hiyo hela tuma kwa Airtel 0698 338 2** Jina BEATRICE KAKUSA. Namba iliyotuma SMS 0697 160 5**. Ajabu mimi pia natumia airtel.

Siku ya jumanne tarehe 4/06/2024 saa nne dakika 35 niliongea na mama yangu ambaye yuko kijijini zilikuwa zinahitajika kutoa kiasi fulani cha hela kwa ajili ya kulipia kibali cha kuhamisha ngómbe toka kata moja kwenda nyingine, ambapo kwa kila ngómbe mmoja ilhitajika shilingi elfu 5.

Ile namaliza tu kuongea na mama saa 4 na dakika 40 meseji ikaingia hiyo hela tuma kwenye namba hii 06987234** jina litakuja Ester Kalinga namba iliyotuma sms 0616 894 5**.

Kutokana na hiyo mifano je niendelee kuamini kuwa hawa watu wabahatisha au Airtel ina watu wanasikiliza mawasiliano yetu na kuwapa matapeli taarifa? Hii tume ya kulinda taarifa ipo kweli na kazi zake ni zipi.
Hizo mambo za sms za kutuma kwenda namba fulani zimebaki kwa Mitandao ya Airtel na Halotel kwa sasa system zao bado hawajaziweka vizuri. Kuwa tu makini.
 
Hizo mambo za sms za kutuma kwenda namba fulani zimebaki kwa Mitandao ya Airtel na Halotel kwa sasa system zao bado hawajaziweka vizuri. Kuwa tu makini.
Wakati zinakuja Randomly sikuwa naona ajabu ila kwa sasa nashangaa kuona kuwa kila nikiongea tu issue ya hela na kukata simu sms inafuata. Kama siyo utaratibu niliyojiwekea na umakini ningeshalizwa sana. Ila utaratibu wangu ukitaka nikutumie hela nipe namba yenye jina lako na si namba uliosajiliwa na mtu mwingine, njia ya pili uende kwa wakala unipe code nitoe hela basi.
 
Back
Top Bottom