Nini kinafanya hoho nyekundu na njano kuuzwa ghali kuliko za kijani?

Evelyn Salt

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2012
Posts
70,916
Reaction score
141,437
Wakulima hizi hoho nyekundu na njano zina nini special ukiachana na rangi za kuvutia, kwanini zenyewe bei iko juu kuliko za kawaida? Soko la ilala mara ya mwisho nlinunua hoho za kijani kilo moja ni elf 3....lakini hoho nyekundu na njano moja inauzwa elf moja.

kwanini ni ghali, au kilimo chake pia ni gharama tofauti na nyingine?

images.jpeg
 
Supply ya hoho za njano na nyekundu ni kidogo wakati demand ni kubwa. Hivyo bei inakuwa juu.
Njano ina vitamin C nyingi kuliko kijani
Nyekundu ina beta carotene nyingi zaidi ya zote
Njano ina zeaxanthin na lutein kiasi kikubwa sana
Njano na nyekundu zinakaa muda mrefu zaidi shambani kabla ya kuvunwa.
 
Okay mkuu.... Tofauti na kuwa zinakaa muda mrefu zaidi shambani bila gharama zake kwenye kuzilima hazina tofauti sana na green. Natamani kuzilima hizi
 
Nahisi za njano na nyekundu zinalimwa kwa lengo la kuwauzia watu wenye uwezo na wa mataifa ya nje.
Ni kama broccoli haziliwi uswahilini na wala hawazijui.

Hivyo hivyo kwa hoho nyekundu na njano kuna watu uswahilini hawajui hata kama zina exist.
 
Licha ya hivyo.....azistawi kirahisi maeneo mengi
Tofauti na species za kijani
 
Ukiona hivyo kuna siri ya nguvu za kiume hapo sio bure
Haya matatizo ya nguvu za kiume, ngoja nizungumze na mwanangu yupo Congo awe analeta vumbi la Kongo, nipige pesa.
 
Nahisi za njano na nyekundu zinalimwa kwa lengo la kuwauzia watu wenye uwezo na wa mataifa ya nje.
Ni kama broccoli haziliwi uswahilini na wala hawazijui.

Hivyo hivyo kwa hoho nyekundu na njano kuna watu uswahilini hawajui hata kama zina exist.
Broccoli🤣 kuna sehemu nliendaga hotel watu wameagiza nikaonja zilikua tamu....namie si nikazinunua kupika zikawa kama dawa🤣🤣 sijawahi kurudia tena kununua.
 
Licha ya hivyo.....azistawi kirahisi maeneo mengi
Tofauti na species za kijani
Inawezekana hii ndio sababu kubwa, kuota kwake ni ishu...nmeulizia mbegu 🙄🙄 gram 10 elf 60 kijani gram 25 elf 4500 hii difference ni Africa na Ulaya 😁
 
Duuh, acha tuendelee kula hiyo CCM na Yanga yetu ya kijani
 
Back
Top Bottom