Nini kinafanya kabila fulani kuwa watani wa kabila lingine?

Nini kinafanya kabila fulani kuwa watani wa kabila lingine?

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Huwa nasikia watu wa kabila fulani anasema kabila fulani ni watani zake, mfano utasikia msukuma anasema mgogo ni mtani wake n.k

Nini kinachopolekea kabila fulani kuwa watani wa kabila lingine?

Unajuaje kabila fulani ni watani wa kabila fulani ?
 
Kuwa na historia ya kusaidiana kwenye matatizo

Vita - hii inatokea sana ikiwa kulikuwa na vita na baada ya muda pande zote zilikubaliana kuimaliza waishi kwa amani

kuruhusu kuoana kwa makabila - inachochea ndugu wa pande mbili kujenga ukaribu na watoto wanakuwa wa pande zote
 
Vita - hii inatokea sana ikiwa kulikuwa na vita na baada ya muda pande zote zilikubaliana kuimaliza waishi kwa amani
Nilipokuwa Ujerumani niliambiwa wahehe na wajerumani wana mkataba kabisa wa utani tena ni documented
 
Nilipokuwa Ujerumani niliambiwa wahehe na wajerumani wana mkataba kabisa wa utani tena ni documented
Utakuwa mkataba feki kama wa Karl Peters na Chief Mangungo, Wajerumani walimsaka sana Mkwawa mpaka akaamua kujipiga risasi
 
Utakuwa mkataba feki kama wa Karl Peters na Chief Mangungo, Wajerumani walimsaka sana Mkwawa mpaka akaamua kujipiga risasi
I do not know lakini walikuwa willing twende kwenye museum tukaone ila sikuwa na muda
 
Tunaishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya mama Samia kwa kuruhusu utani wa makabila.
 
Pia kuwa majirani pia sababu ya kuwa watani pia kwa mfano walugulu na wa wasambaa tanga,wachaga na wa tanga kigoma sumbawanga na mengine
 
Back
Top Bottom