Nini kinakuzuia usianzishe biashara?

Masokotz

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2018
Posts
3,713
Reaction score
6,121
Habari za wakati huu,

Ni matumaini yangu kwamba unaendelea vyema na maisha yako ukiendelea kuzifikia ndoto zako.Katika safari yangu ya ujasiriamali na biashara ambayo ina umri wa zaidi ya miaka 20 ni mefanya aina nyingi sana za biashara. Nimefanya biashara ya maduka ya nguo,maduka ya chakula, Biashara ya bar na hata biashara ya jiko la chipsi n.k.utoaji wa huduma mbalimbali,maduka ya spea za magari,pikipiki hata nimefanya biashara katika sekta ya elimu na hata udalali wa nyumba na mashamba.

Najua unaweza kushangaa inakuwaje nimefanya biashara za aina nyingi hivi?Well katika maisha kuna hatua na katika kila hatua unajikuta unakumbana na hustles ambazo zinakufanya uingie katika aina fulani ya biashara kwa muda mfupi au muda mrefu. Najua siko mwenyewe ambaye ninafanya biashara za aina tofauti ila najua kuna watu ambao kabisa hawajawahi hata kujaribu kufanya biashara. Swali la kujiliza ni JE nikitu gani kinakufanya na wewe usianzisha kabiashara kako hata kama ni kadogo?Je ni Mtaji?Je ni wazo la biashara huna?Je ni muda?Je ni uwezo wako wa kiakili ni mdogo?Je ni fursa hauzioni?Ni kitu gani kinakuzuia kufanya biashara?

Kila mtu anazo sababu zinazomfanya asianzisha biashara.Ila leo nataka nikwambie ni kwa nini ni muhimu uanzisha kabiashara kako.Hata kama ni kadogo.Siku hizi kuanzisha biashara ni rahisi sana.Kuendesha na kusimamia biashara ni rahisi sana.Unapokaa bila kuwa na Biashara unapishana na FURSA ambazo utakuja kuzikumbuka.

Jaribu kufikiri kampuni kama za FACEBOOK(META),GOOGLE(ALPHABET),TWITTER,TIKTOK na kampuni nyingine kama hizo halafu ujiulize iwapo zina tofauti yeyote.Hizi zote ni kampuni za TEHAMA ambazo kiuhalisia zinadeal na Taarifa tu.Ni kampuni ambazo ni kubwa sana na zinaingiza mabilioni ya PESA.Swali ni JE unafikiri uanzishwaje wake ulikuwa mgumu au mrahisi?

Ukizitazama hizi kampuni unaweza kufikiri kuzianzisha ilikuwa kazi ngumi il ilikuwa kazi rahisi sana.Ilifanywa na mtu mmoja au wawili ambao waliamini katika wazo lao na kutenga muda na rasilimali zao kulipa wazo lao nguvu.Baada ya hapo sote tunajua kilichotokea.

Biashara yoyote inaanza na wazo na kuliamini wazo lako.Mawazo ya biashara yako mengi na yote yanaweza kukuingizia kipato tena cha kutosha kabisa. Swali la kujiuliza ni Je unaliamini wazo lako?Hapo ndipo ambapo wengi wetu hukwama. Kwani sisi wenyewe tunakuwa hatuamini katika wazo na uwezo wetu na matokeo yake ni kwamba tunapokutana na changamoto yoyote ni rahisi kufikiri kwamba tumefikia Mwisho kumbe bado ni mwanzo tu.

Wazo lolote la biashara ni lazima ulifanyie "Validation" Hii unaweza kufanya kwa kuangalia wengine wanafanya nini katika eneo hilo au unaweza kulipeleka sokoni kwa baadhu ya wateja ili uone iwapo litawafaa na unaweza.Kumbuka usipolifanyia wazo lako validation ni vigumu sana wewe kuelewa kwa kina aina ya biashara na changamoto zake.

Katika mjadala huu nimechokoza kidogo tu kuhusu kile kinachotuzuia kuanzisha biashara na namna ambavyo tunaweza kuvuka changamoto.Hata hivyo naamini kwamba yako mengi ambayo yanawazuia watu wasianzishe biashara. Karibuni tujadili kwa pamoja Juu ya yale ambayo yanatuzuia kuanzisha biashara na namna ambavyo tunaweza kuyashinda na kuibua mawazo na fursa mpya.

Karibuni
 
Kweli boss lakini chamusingi tujue dunian tuko watu wawili tofauti asa kwenye msingi waajila kuna aliye zaliwa kuajiliwa uyu simshauli kuazisha biashara na aliyezaliwa kuajili uyu aazishe atagenge lakuuza nyanya.
 
Kweli boss lakini chamusingi tujue dunian tuko watu wawili tofauti asa kwenye msingi waajila kuna aliye zaliwa kuajiliwa uyu simshauli kuazisha biashara na aliyezaliwa kuajili uyu aazishe atagenge lakuuza nyanya.
Mkuu,wote tunaweza anzisha biashara.Kama huwezi kuanzisha biashara basi hata kuajiriwa hutofaa.
 
Biashara si lelemama,hasa kwenye nchi zetu hizi za Dunia ya tatu,ambako rushwa utawala.

Lakini pamoja nanugumu huo ni muhimu kujitoa muhanga,lazima uchukue maamuzi ya wakoma,kwamba ukibaki bila biashara unakufa lakini ukiamua kutumbukiza ka mtaji uliko Nako waweza kukapoteza au ukapata faida mara dufu.

Wengi wanashindwa kuanzisha biashara kwa sababu wanahofia ikiwa biashara itakufa na hiyo ndo akina waliyonayo atakuwa mgeni wa nani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…