Nini kinakwamisha 'Hakimiliki' katika sanaa ya Tanzania

Uchunjuba Punjubi

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2017
Posts
799
Reaction score
622
Habarini wakuu, kwa muda sasa wasanii hapa Tanzania wamekuwa wakilalamika kuhusu kitu kinaitwa HAKIMILIKI na imekuwa shida sana kufanikiwa, kila siku wanapigwa danadana, shida hasa imekuwa wapi? Kama sheria hakuna kwa nini isitungwe, kwa maana sanaa imekuwa ni ajira ambayo inatakiwa kurasimishwa sasa. Pia nataka kujua ni nani anatakiwa kushughulikia hili swala ili wasanii wapate haki yao? Anakwama wapi? Msaada wenu tafadhali ili nijue.
 

Hakimiliki ni automatic, yaani ukitoa tu kazi yako tayari inalindwa. Ni nchi chache duniani ambazo zinahitaji hakimiliki zisajiliwe. Tanzania hazisajiliwi, hivyo hakuna anayekwamisha hakimiliki za wasanii tanzania. Mtihani upo jinsi wasanii wanavyotambua kwamba kazi zao zina hakimiliki na jinsi ya kunufaika na hizo kazi. Nawasilisha
 
Asante mkuu, kwahiyo ipo sheria inayowalinda kiasi kwamba wakimkuta mtu anauza kazi zao ovyo wanaweza kuwashitaki?
 
Asante mkuu, kwahiyo ipo sheria inayowalinda kiasi kwamba wakimkuta mtu anauza kazi zao ovyo wanaweza kuwashitaki?

Tanzania sheria ipo na inawalinda. Tatizo ni kupata ushahidi, maana unaweza kwenda mshitaki mtu na yeye akaruka. Polisi wetu mambo wa hakimiliki hawajui, hivyo wao kwenda moja kwa moja kumkamata mtu inakuwa ni vigumu. Ndio maana wasanii wanashauriwa wajiunge na COSOTA naamini COSOTA wanakitengo kinachohusika na masuala ya hakimiliki na wanaweza saidia kutumia vyombo vya dola kwenda kumkamata na kumshitaki anayeuza kazi za msanii husika bila kibali.
 
Sawa sawa mkuu
 
Tofauti ya HAKIMILIKI na HATIMILIKI ni nini?

Hatimiliki inahusiana na umilikaji wa physical property hususan ardhi

hakimiliki inahusiana na umilikaji wa intellectual property hususan copyright
 
Tatizo sio Hakimiliki bali sheria zinazoshughulikia violations of Hakimiliki!

Naamini sheria zinazoshughulikia violation ya Hakimiliki zipo bali tatizo kubwa lipo kwenye vyombo vinavyopaswa kusimamia na kutekeleza sheria hizo. Sina hakika mahakama zetu au mahakama za biashara zina mahakimu wenye ujuzi eneo hilo la hakimiliki na "intellectual property" katika ujumla wake, vivyo hivyo polisi, forodha n.k.
 
Hatimiliki inahusiana na umilikaji wa physical property hususan ardhi

hakimiliki inahusiana na umilikaji wa intellectual property hususan copyright
Kwahiyo Copyright kwa kiswahili ni hakimiliki? Unatoa maelezo haya kama wewe ni mtaalamu au unaongea tu ujuavyo?
 
Tatizo sio kuwepo hizo sheria bali uzito wa sheria zenyewe! Kwa mfano, mtu anaweza kukutwa na hatia ya kudurufu kazi za sanaa lakini faini yake ni kichekesho!

Matokeo yake watu hawaogopi kudurufu kazi za wasanii kwa sababu wanafahamu hata wakidakwa, hukumu yake ni ndogo sana! Ni kutokana na hilo ndio maana nikasema tatizo ni sheria zinazoshughulikia copyright violations!! Uzuri wa sheria watu waogope kutenda kosa kwa hofu ya sheria inayoshughulikia kosa husika!

Leo hii ukikutana na 16 years school girl, unajua kabisa mikikimikiki ya dushe anaihimili bila tatizo lakini ukifikiria miaka 30 hapo hapo dushe linasinyaa!
 

Kwa hilo nakubaliana nawe kabisa. Adhabu ni finyu sana na haiogopeshi. Swali ni je tunarekebishaje hali hii? Huo mfano wako wa 16yrs ni noma 😀
 
Kwa hilo nakubaliana nawe kabisa. Adhabu ni finyu sana na haiogopeshi. Swali ni je tunarekebishaje hali hii? Huo mfano wako wa 16yrs ni noma 😀
Cha kufanyika kipo lakini nahisi mapigo ya moyo kwenda mbio kila nikifikiria nini kinatakiwa kufanywa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…