SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Moja ya mambo yanayokwamisha sana mpira wetu ni ushindani na uhasama wa Simba na Yanga unaopelekea vilabu hivi siyo tu kushindwa kushirikiana katika mashindano ya kimataifa bali wakati mwingine hadi kuhujumiana na kufanyiana fitna.
Juzi juzi nilipokuwa naangalia tuzo za CAF niliona jinsi wenzetu wanavyojivunia sana mchezaji au timu yao iwe klabu au ya taifa inapofanikiwa na kupewa matuzo. Pamoja na kwamba nchi nyingi zina timu zenye upinzani wa jadi, sina uhakika kama huwa wanadhihakiana pale mmoja anapofanikiwa katika jambo lake.
Najua katika uhalisia wa utani wa jadi wengine wanasema ni tunu ya taifa inayoendelea kuimarisha umoja wetu, wengine wanasema inasaidia kunogesha mpira na maisha yetu. Inawezekana yote haya yana ukweli fulani.
Binafsi naona bila ushirikiano fulani wa kimkakati kati ya vilabu hivi itakuwa ngumu sana moja ya vilabu hivi kutoboa kimataifa maana unaweza sogea kidogo halafu mwenzio atakukwamisha tu, halafu unamuona yuleee pale jukwaani anashangilia anguko lako. Huu uhasama na utani wa jadi unacheza katika mstari mwembamba wa chuki na wivu kwa upande mmoja na utani kwa upande mwingine.
Unadhani nini kifanyike kutengeneza mkakati wa kushirikiana au kama hauwezi kumsaidia mwenzio basi angalau usimuwekee vigingi katika njia yake?