Black Legend
Senior Member
- Jul 28, 2015
- 174
- 301
Kama mdau wa maendeleo wa nchi hii yetu pendwa..nimekua toka enzi za utoto nikiona matumizi makubwa ya RELI ya TAZARA. Katika utawala wa Mwinyi na Mkapa RELI hii ilikuwa ni kitovu cha uhudumiaji nchi za ukanda wa kusini kama Zambia, Malawi, Congo DR nk.
Abiria na mizigo Mingi ilisafirishwa kupitia RELI hii. Pale Mbeya kulikuwa center kubwa ya kupakua mizigo kama Magari na pia mafuta yalihifadhiwa pale kwenye matanki makubwa kwa nchi kama MALAWI chini ya kampuni maarufu ya serikali ya Malawi MALAWI CARGO nk.
Kwa utawala wa Kikwete, Magufuli na Sasa Samia, hii RELI ni kama imekufa na hakuoneshi juhudu za dhati za kuboresha na kuirudisha katika ufanisi wake hii RELI.
Mikoa ya kusini na nchi za kusini mwa Tanzania ni wahudumiaji wakubwa wa uchumi wa nchi yetu.....kuwa na huduma imara ya RELI TAZARA kungeleta tija kubwa saana kwenye nchi yetu.
KWA RAIS WA NCHI NA WASAIDIZI WAKE(MAWAZIRI, WABUNGE NK.) NI WAKATI MUAFAKA SASA KULITAZAMA HILI SUALA KWA JICHO LA KIPEKEE, KAMA TUNATAKA NCHI IPAE KWA UCHUMI IMARA,HATUNA BUDI KUIMARISHA TAZARA....."It can be done, let's play our part". 🙏🏼🙏🏼🙏🏼🇹🇿