Nini kinamsumbua huyu ndugu?

K-Boko

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2013
Posts
697
Reaction score
218
Jamaa ni ME. Anasema usiku kwake ni shida tupu. Kila mara anapojaribu kulala anahisi kuzingirwa na hali fulani inayoambatana na joto la kiwango fulani na kisha anahisi kuingiliwa sehemu za haja kubwa. Nafuu yake ni kunyanyuka kitandani haraka na kukaa akiwaza kinachomsibu! Matokeo yake anakosa usingizi kwa muda mrefu na siku zinavyoendelea inamuathiri sana kiafya. Mimi nimenawa naona giza tu. Anahitaji msaada wa kweli kweli angalau wa mawazo tu.
 
duh, usije kuwa ni wewe mkuu, pole sana. nenda kanisani kaombewe. usijejikuta umekuwa binadamu wa ajabuajabu.
 
...jini mahaba,suluhisho ni Yesu tu...
 
duh, usije kuwa ni wewe mkuu, pole sana. nenda kanisani kaombewe. usijejikuta umekuwa binadamu wa ajabuajabu.

Hahaahaaa! Nami nasaidia tu kama wewe unavyosaidia mzee.
 
kama ni muislam kila siku ahakikishe usiku anasoma suratul Baqra, hakika yataondoka kabisaa hayo yanayomsibu.
au kama hajui kusoma chochote afanyiwe rukya ya kisheria sio kwenda kwa waganga.
Ila kama ni mkristo hapo siwezi kusema wengine watasaidia
 

MJUE JINI MAHABA NA DALILI YAKE






NI NANI JINI MAHABA (AASHIQ DJINN )

unapoongelea juu ya jini mahaba basi unaongelea jambo muhimu na gumu, kwani majini wapo aina karibia 660, na kila jamii ina kuwa na mifumo yake pindi awapo mahaba.
jini mahaba si jini maalum kusema huyu ni mahaba,
mfano sisi binaadamu hatuna kabila maalumu kwamba hawa ni watu tabia mbaya, ila tabia mbaya huwa kwa mtu mwenyewe ni kwa kabila.
pia jini mahaba si jini maalum kuwa huyu ni mahaba ila majini wote waoi wahuni miongoni mwao ambao husumbua maisha ya wanadamu.


DALILI ZA KUJUA UNA JINI MAHABA




1) Kuwa na hasira zisio na sababu


2) kutokuwa hamu ya jimai

3) kupata maumivu na na michubuko katika jimai

4) kuchoka sana wakati wa jimai.

5) kumchukia mwenza wako pindi anapo kuwa karibu na wewe.
huyu ni JINI SUBIANI.

6) kukosa hedhi


7) kupata hedhi kwa miezi miwili hadi mitatu

8) kuumwa chango au ngiri mara kwa mara

9) kushindwa kumwaga manii ufanyapo jimai

10) kuingia na kumwaga manii haraka sana
huyu ni jinni UMMU MULDAMI.

11) kupoteza ladha ya jimai katikati ya tendo


12) kuishiwa nguvu haraka

13) kupatwa maumivu makali ya tumbo wakati ukifanya jimai

14) Kuto kuona ladha yeyote na mwanamke kushindwa kutoa ute na kumpa maumivu
huyu ni JINI JALWUSH

15) Kuto kubeba mimba


16) Kujaa maziwa kama mjamzito

huyu ni UMMU SUBIANI

17) Kuota Unapaa


18) Kuharibika Mimba kaabla ya Miezi Minne

19) Chunus zisizo SIKIA DAWA

20) Kuchukia kutongozwa na kuto hitaji ndoa
huyu ni JINI TWAYR {qarnail}

21) Kuto tosheka na jimai

huyu ni MAYMUNA

22) Mtoto kumuogopa mama yake



23) Kuota unafanya mapenzi


24) Mama kuto toa maziwa akijifungua


25) Mtoto kupatwa degedege.

huyu ni MAKATA WA MAKATANI.



26)Kuota unamuingilia Mwanamke au Mwanamke anaingiliwa usingizini.

Ukitaka dawa zake nione mimi kwa kubonyeza hapa.
Mawasiliano
 
Sawa. Lakini mfano akiniuliza sababu ya kupatwa na hayo majini je?
 
kama ni muislam kila siku ahakikishe usiku anasoma suratul Baqra, hakika yataondoka kabisaa hayo yanayomsibu.
au kama hajui kusoma chochote afanyiwe rukya ya kisheria sio kwenda kwa waganga.
Ila kama ni mkristo hapo siwezi kusema wengine watasaidia

Ahsante salam zimefika. Sorry lakini, rukya ndio nini?
 
Ruqyah maana yake ni usomaji wa Qur-aan na uombaji wa dua kwa Allah (Subhaanahu wa Ta'ala) ili kupata msaada wake katika tiba ya ugonjwa na matatizo mengine na haihusiani kabisa na mambo ya uganga.
 
Taratibu Za Ruqyah Na Yapasayo Kufanywa Kabla Ya Kusoma Ruqyah.

watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako hilo kuhusu Ruqyah. Katika mas-ala ya Ruqyah zipo Aayah za kusomwa na mtu mwenyewe za kutaka kinga kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta‘ala) na zipo zile za kumsomea mtu aliyekumbwa na jini au kufanyiwa sihri.

Ama njia ya kujikinga mwenyewe ni kuwa uwe unasoma Aayah zifuatazo asubuhi na jioni. Nazo ni kama zifuatazo:


1. Al-Faatihah (Surah ya kwanza).
2. Al-Baqarah (Aayah nne za mwanzo, Ayatul Kursiy na Aayah mbili baada yake na Aayah tatu za mwisho).
3. Aal-‘Imraan (3: 1 – 2).
4. Suratut Tawbah (9: 129 mara saba).
5. Al-Israa' (17: 110 – 111).
6. Al-Mu'minuun (23: 115 – 118).
7. Al-Hashr (59: 22 – 24).
8. Al-Kaafiruun (109).
9. Al-Ikhlaasw, al-Falaq na an-Naas (mara tatu tatu).



Ama kipengele cha pili cha kumsomea mwengine inafaa usome Aayah zifuatazo:

Mwanzo unaanza na A'udhu Billaahi minash Shaytwaanir Rajiym.
1. Al-Faatihah (Surah ya kwanza).
2. Al-Baqarah (ayah 1 – 5, 102, 163 – 164, 255, 285 - 286).
3. Aal-‘Imraan (3: 18 – 19).
4. Suratut al-A‘raf (7: 54 – 56, 117 - 122).
5. Yunus (10: 81 – 82).
6. Twaaha (20: 69).
7. Al-Hajj (22: 19 – 22).
8. Al-Mu'minuun (23: 115 – 118).
9. An-Naml (27: 30 – 31).
10. Asw-Swaaffaat (37: 1 – 10).
11. Ad-Dukhkhaan (44: 43 – 48).
12. Al-Ahqaaf (46: 29 – 32).
13. Al-Fath (48: 29).
14. Ar-Rahmaan (55: 33 – 36).
15. Al-Hashr (59: 21- 24).
16. Al-Jinn (72: 1 – 9,
17. Al-Buruuj (85).
18. Zilzalah (99).
19. Al-Humazah (104).
20. Al-Ikhlaasw, al-Falaq na an-Naas.

Ama unapokuwa unasoma unafaa uwe twahara (nguo na mwili) na umejisitiri kwa kujifunika vizuri sehemu zipasazo kusitiriwa na pia usome kwa unyenyekvu.

Na Allaah Anajua zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…