Taratibu Za Ruqyah Na Yapasayo Kufanywa Kabla Ya Kusoma Ruqyah.
watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako hilo kuhusu Ruqyah. Katika mas-ala ya Ruqyah zipo Aayah za kusomwa na mtu mwenyewe za kutaka kinga kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta‘ala) na zipo zile za kumsomea mtu aliyekumbwa na jini au kufanyiwa sihri.
Ama njia ya kujikinga mwenyewe ni kuwa uwe unasoma Aayah zifuatazo asubuhi na jioni. Nazo ni kama zifuatazo:
1. Al-Faatihah (Surah ya kwanza).
2. Al-Baqarah (Aayah nne za mwanzo, Ayatul Kursiy na Aayah mbili baada yake na Aayah tatu za mwisho).
3. Aal-‘Imraan (3: 1 – 2).
4. Suratut Tawbah (9: 129 mara saba).
5. Al-Israa' (17: 110 – 111).
6. Al-Mu'minuun (23: 115 – 118).
7. Al-Hashr (59: 22 – 24).
8. Al-Kaafiruun (109).
9. Al-Ikhlaasw, al-Falaq na an-Naas (mara tatu tatu).
Ama kipengele cha pili cha kumsomea mwengine inafaa usome Aayah zifuatazo:
Mwanzo unaanza na A'udhu Billaahi minash Shaytwaanir Rajiym.
1. Al-Faatihah (Surah ya kwanza).
2. Al-Baqarah (ayah 1 – 5, 102, 163 – 164, 255, 285 - 286).
3. Aal-‘Imraan (3: 18 – 19).
4. Suratut al-A‘raf (7: 54 – 56, 117 - 122).
5. Yunus (10: 81 – 82).
6. Twaaha (20: 69).
7. Al-Hajj (22: 19 – 22).
8. Al-Mu'minuun (23: 115 – 118).
9. An-Naml (27: 30 – 31).
10. Asw-Swaaffaat (37: 1 – 10).
11. Ad-Dukhkhaan (44: 43 – 48).
12. Al-Ahqaaf (46: 29 – 32).
13. Al-Fath (48: 29).
14. Ar-Rahmaan (55: 33 – 36).
15. Al-Hashr (59: 21- 24).
16. Al-Jinn (72: 1 – 9,
17. Al-Buruuj (85).
18. Zilzalah (99).
19. Al-Humazah (104).
20. Al-Ikhlaasw, al-Falaq na an-Naas.
Ama unapokuwa unasoma unafaa uwe twahara (nguo na mwili) na umejisitiri kwa kujifunika vizuri sehemu zipasazo kusitiriwa na pia usome kwa unyenyekvu.
Na Allaah Anajua zaidi