Nini kinapelekea utofauti wa miaka ya kuhitimu shahada ya uuguzi na ukunga Tanzania ikiwa vyombo husika vinaelekeza miaka 4?

Nini kinapelekea utofauti wa miaka ya kuhitimu shahada ya uuguzi na ukunga Tanzania ikiwa vyombo husika vinaelekeza miaka 4?

Ewhite

New Member
Joined
Nov 2, 2026
Posts
3
Reaction score
2
Kwa Tanzania kada ya Uuguzi na Ukunga ngazi ya Shahada(Degree) inasomwa miaka 4 ukiongeza mmoja wa intership,lakini kwa masikitiko ni kwamba kuna baadhi ya vyuo sitavitaja vinatoa iyo shahada kwa miaka 3 wengine miaka 2.5
Ni kwanini Baraza la Uuguzi na Ukunga(TNMC) limeshindwa kusimamia hii sera ya kusoma shahada miaka 4 na badala yake limekaa kimya kama hakuna kinachotokea?

Athari zake;Kutokana na kutokuwepo Uniformity ndani ya kada wauguzi waliosoma miaka 4 ya shahada wameshindwa kupata haki yao ya msingi ya kuanza mshahara ngazi ya TGHS D badala yake wanaanza na C!!
Ni nini kazi ya TNMC kama wameshindwa kusimamia walichokianzisha??
 
Back
Top Bottom