Nini kinasababisha wake za marafiki zangu wawili Joni wa Kanda ya Ziwa na Huseni wa Visiwani Zanzibar mmoja kuwa Mchangamfu na mwingine Mpweke?

Nini kinasababisha wake za marafiki zangu wawili Joni wa Kanda ya Ziwa na Huseni wa Visiwani Zanzibar mmoja kuwa Mchangamfu na mwingine Mpweke?

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2015
Posts
8,018
Reaction score
16,802
Na kinachonishangaza zaidi Joni ni mkubwa Kiumri na hata Kipesa kuliko Huseni ila cha Kushangaza ni Siku chache sana tu Huseni wa Visiwani Zanzibar kapanda Cheo cha Kusimamia Karafuu za Zanzibar huku akitanguliwa Siku nyingi na Joni ambaye ana Cheo cha Kusimamia Samaki zote za Kanda ya Ziwa ila Mke wa Huseni Pichani anaonekana Kuchangamka tofauti na Mke wa Joni

Je, tofauti hii inatokana na nini labda? Naombeni Ushauri wenu kwani wote Wawili pamoja na Rafiki yetu wa Hiari Sefu natarajia Kukutana nao katika Kupata Chanjo mpya ya CORONA kutoka Mgeni wetu na Rafiki yetu wa Siku nyingi mno kutokea China ambako ametuletea ila kutokana na Hali ya Hewa ya Dar es Salaam na Dodoma kuwa mbaya kwa sasa ameshauri tukachanjiwe Kanda ya Ziwa huko.

Na nategemea pia nikiwa huko Kanda ya Ziwa napata Chanjo ya CORONA nitakutana nao hawa Wake na wa Rafiki yangu mwingine nae Kasimu Yeye najua Wiki ijayo nae tutakuwa nae kwani huyu Rafiki yetu Mchina anatupenda sana na kasisitiza tuipate upesi hii Chanjo na tuweze kumpa mrejesho ili kama vipi aweze Kutuagizia na zingine kwa ajili ya wana Familia wetu ambao wanafikia Milioni 55 Kiujumla.
 
59995389_171865653812008_4640147993603866624_n.jpg
 
Mambo ya wake za watu hatuna muda nayo ila tuambie wewe habari za umalaya wa mkeo.
 
Mambo ya wake za watu hatuna muda nayo ila tuambie wewe habari za umalaya wa mkeo.
Wenye Akili timamu na wanaojua kufungua vyema kabisa Codes nina uhakika hapa wamekielewa nilichokimaanisha ila Wapumbavu mmepotea tu.
 
Wenye Akili timamu na wanaojua kufungua vyema kabisa Codes nina uhakika hapa wamekielewa nilichokimaanisha ila Wapumbavu mmepotea tu.
Fumbo fumbia mjinga mwerevu atang'amua tu hapo hakuna code yoyote kwakuwa umewataja watu moja kwa moja na maeneo wanayotoka na wanayoongoza sasa utasema ujumbe wako ni coded?
 
Fumbo fumbia mjinga mwerevu atang'amua tu hapo hakuna code yoyote kwakuwa umewataja watu moja kwa moja na maeneo wanayotoka na wanayoongoza sasa utasema ujumbe wako ni coded?
Haoni Uzi wake umechacha sijui.
 
Back
Top Bottom