Nini Kipi Muhimu "LOVE" au "TRUST"?

Nini Kipi Muhimu "LOVE" au "TRUST"?

Superman

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2007
Posts
5,693
Reaction score
1,702
Kuna aina nyingi za Mapenzi. Kuna mapenzi ya Mama na mwanae, family members, marafiki n.k. Mapenzi ya namna hii huwa yanatokea au kuanza bila kuwepo na condition ya TRUST.

Kumekuwa na mijadala katika mapenzi ambayo yanahusisha mwenzi wa jinsia nyingine (Romantic Love). Je mapenzi ya namna hii yanahitaji TRUST?

Kama hayahitaji TRUST, iwaje moja katika mahusiano anapogundua mwenzi wake si MWAMINIFU anumia sana (Heart Broken?)

Ni nini muhimu hasa katika Mapenzi na nikipi ni muhimili mkubwa wa mapenzi kwa Wapenzi Wapya au wa siku nyingi?: LOVE au TRUST?

Tushauriane huku tukitoa sababu za msingi ikiwezekana na mifano.
 
Kwanza kabisa mapenzi na uaminifu ni vitu viwili tofauti!Kimoja hakiwezi kuchukua nafasi ya mwenzake hivyo huwezi kuchagua kipi ni bora!Kwa wapenzi mapenzi na kuaminiana vinaenda pamoja!Hamna ambacho ni muhimu zaidi ya mwenzake kwasababu vinategemeana in a way!Ukimpenda mtu bila kumuamini ni rahisi kupoteza yale mapenzi..na kumwamini mtu usiempenda haitoshi kuwafanya wapenzi!
 
Vyote ni muhimu mkuu, haina maana umpende mtu then usimwamini, we mpende tuu na mwamini afu tegemea the same,,, ila usimpe namba zako za siri za ATM card yako!
 
Wenzi wanapokuwa wapya ni kipi kinaanza? Au vinaanza kwa pamoja?

Tunaambiwa na wanandoa kuwa LOVE huchuja au hufifia na kubaki mazoea; je TRUST nayo je?

Ni kwa vipi hivi vinaenda pamoja?
 
Vyote ni muhimu mkuu, haina maana umpende mtu then usimwamini, we mpende tuu na mwamini afu tegemea the same,,, ila usimpe namba zako za siri za ATM card yako!

Unaamua kumpenda mtu na kumwamini; then unaguandua kuwa anacheat; je LOVE itakuwepo bado?

Na kama huwezi kumpa pin ya ATM je kuna Trust hapo?
 
Je; kwa wapenzi wapya ambao wanadai kuwa wanapendana? W Je kuna moja anaweza akakosa kum-TRUST mwenzake kwa sababu yoyote na mapenzi bado yakawepo?
 
kuna aina nyingi za mapenzi...
ukimpenda mwanao wa miezi miwili huitaji trust
lakini romantic love lazima iendane na trust mkuu
ndo maana watu wanapokuwa cheated on wanaumia sana...
 
kaka mm nnafkr tatzo lipo kwny uaminifu ukiona uaminifu umeshuka kaa ukijua kuwa upendo haupo tena so uaminifu ni ki2 cha mcng sana katka mausiano kama unamjal mwenzako hakika utakuwa mwaminifu kwake na upendo utaongezeka pia so trust kwnz alafu love bidae
 
kuna aina nyingi za mapenzi...
ukimpenda mwanao wa miezi miwili huitaji trust
lakini romantic love lazima iendane na trust mkuu
ndo maana watu wanapokuwa cheated on wanaumia sana...

Kwa hiyo ni sawa kusema bila TRUST hakuna LOVE?

Au bila LOVE hakuna TRUST?
 
kaka mm nnafkr tatzo lipo kwny uaminifu ukiona uaminifu umeshuka kaa ukijua kuwa upendo haupo tena so uaminifu ni ki2 cha mcng sana katka mausiano kama unamjal mwenzako hakika utakuwa mwaminifu kwake na upendo utaongezeka pia so trust kwnz alafu love bidae

Nimekusoma Mkuu;

Loud and clear kuwa NO TRUST; NO LOVE. Ngoja tuwasikie na wengine.
 
Vyote kwa pamoja!Ndo maana unakuta mtu anampenda mtu hata hamjui sana..moyo unaamua kujitoa kwa huyo mtu bila sababu maalumu kwa kua anamwamini kiasi cha kumpa moyo wake!Alafu unavyouliza kama Trust hufifia kwani hujui kwamba mtu anaweza kukuamini bila wewe kumpa sababu ila kutokumuamini mtu kunaletwa na sababu!?So ndio jibu ni ndio Trust inaweza kufa.Kuhusu mapenzi kufifia nayo inawezekana..ila mazoea hayawezi kuchukua nafasi ya mapenzi!
 
Mkuu hapo umechanganya mambo
unaweza ukampenda mtu bila kumuamini kabisa, mfano hata akikucheat its not necessary kwamba upendo wako kwake utakwisha

Now unaweza ukamuamini mtu na usimpende, ila kwenye relationship trust ni muhimu ili relationship idumu kwa muda mrefu, sababu bila trust kutakuwa na wivu wa ajabu ajabu ambao utapelekea watu kuachana..

Therefore to answear your question huitaji trust kupenda mtu, huitaji love ku-trust mtu BUT kwenye relationship to blossom you need both trust and love
 
Wenzi wanapokuwa wapya ni kipi kinaanza? Au vinaanza kwa pamoja?

Tunaambiwa na wanandoa kuwa LOVE huchuja au hufifia na kubaki mazoea; je TRUST nayo je?

Ni kwa vipi hivi vinaenda pamoja?
mkianza mapenzi itaanza trust. Kama sikutrust sitokuwa tayari kufanya chochote na wewe.
Nimekuamini ndio maana nimekupa moyo wangu.

Kuhusu penzi kuchuja ni pale uaminifu unapoisha.
Kama kila siku nahisi unacheat hata sitokuonesha mapenzi ya dhati. Tutakuwa tupo tupo tu na hatimaye ndoa itavunjika.
Vinaenda kwa pamoja kwasababu unayempenda kwa dhati lazima utamuamini.
 
unaweza ukampenda mtu bila kumuamini kabisa, mfano hata akikucheat its not necessary kwamba upendo wako kwake utakwisha
upendo unaisha VOR na ndio maana watu waliofumaniana huwa ni ngumu kurudia mahusiano na wakaishi kama zamani.
 
upendo unaisha VOR na ndio maana watu waliofumaniana huwa ni ngumu kurudia mahusiano na wakaishi kama zamani.

hawawezi kuishi kama zamani sababu hakuna Trust, na ndio maana nikasema bila Trust hakuna uhusiano wa kudumu, lakini unaweza ukampenda mtu anayekuumiza, mtu anayekudanganya kila siku, sababu ya penzi kubwa unajipa moyo labda atabadilika.., lakini kama nilivyosema Love inahitaji mazingira fulani, sasa kama mmea bila mbolea au maji basi mmea huo utakufa.., kwahiyo kwa love kufa sio trust tu ni mambo mengi yanayoweza kupelekea love ikaisha.., ila nimeshaona watu wanapenda hadi wanakuwa vipofu hata wakifanyiwa nini bado wataendelea kupenda tu.
 
Back
Top Bottom