1 Wakorintho 13
Upendo
1Kama ningekuwa na uwezo wa kusema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa kama kelele ya kengele au toazi.
2Na kama nina uwezo wa unabii, na kuelewa siri zote na maarifa yote; na hata kama nina imani kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, mimi si kitu.
3 Kama nikitoa mali yote niliyo nayo, na kama nikitoa mwili wangu uchomwe moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu.
4Upendo huvumilia, upendo hufadhili; upendo hauna wivu au majivuno.
5Upendo hauna kiburi na haukosi kuwa na adabu. Upendo hau tafuti kujipendeza nafsi; haukasiriki upesi, hauweki orodha ya mabaya.
6Upendo haufurahii mabaya, bali hufurahia kweli.
7Upendo huvumilia yote, huamini yote, hutumaini yote, hustahim ili yote.
8Upendo hauna mwisho. Lakini penye unabii, utakoma; zikiwepo lugha zitakoma; yakiwepo maarifa yatakwisha.
9Kwa maana tunafa hamu kwa sehemu na tunafanya unabii kwa sehemu.
10Lakini uka milifu utakapokuja, yale yasiyo kamili yatakwisha.
11Nilipokuwa mtoto mdogo, nilisema kama mtoto mdogo, niliwaza kama mtoto mdogo, nilifikiri kama mtoto mdogo. Nilipokuwa mtu mzima niliacha mambo ya kitoto.
12Kwa maana sasa tunaona sura kama ya kwenye kioo, lakini wakati huo tutaona uso kwa uso. Sasa nafahamu kwa sehemu, wakati huo nitafahamu kikamilifu, kama vile ninavyo faha mika kikamilifu.
13Basi sasa, mambo matatu yanadumu: imani, tumaini na upendo. Lakini lililo kuu kati ya haya ni upendo.