Kijukuu cha Tanzania
Member
- Dec 6, 2025
- 7
- 5
Katika hali ya kushangaza, ni takribani mwaka mzima sasa fremu nyingi zimefungwa na hazitumiki licha ya kuwepo kwa uhitaji mkubwa kutoka kwa wananchi.
Ukifuatilia zaidi, unaambiwa fremu hizo zipo mikononi mwa wahusika ambao hawatajwi wazi. Aidha, kabla ya kupangishwa, unatakiwa uandae zaidi ya shilingi milioni nne ili kuwapa watu wanaodaiwa kuzimiliki; ndipo uweze kupata fremu.
Najiuliza ni akina nani wanaomiliki fremu hizo, na kwa nini zinashindwa kufanya kazi licha ya nyingi kukamilika. Je, Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni haioni changamoto hii kuwa inazorotesha mzunguko wa watu na maendeleo katika stendi hiyo?
Ninatoa wito kwa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni pamoja na TAMISEMI kufuatilia suala hili. Ikiwa kuna mazingira ya “upigaji”, wahusika wawajibishwe na fremu hizo zianze kutumika ili kuchochea mzunguko katika eneo hilo.