Nini kipo nyuma ya pazia mfululizo wa misukosuko ya Chadema?

DodomaTZ

Senior Member
Joined
May 20, 2022
Posts
197
Reaction score
233
Katika siasa, mara nyingi matukio makubwa huanza kama ishara ndogo, lakini zenye ujumbe mzito uliojificha ndani yake.

Kwa kipindi cha takribani mwaka mmoja sasa, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimekuwa kikikabiliwa na mfululizo wa matukio mbalimbali hasa misukosuko ya kisiasa na kisheria ambayo kwa watazamaji wengi wa medani ya siasa sio matukio ya kawaida. Hasa yanapojitokeza katika mazingira yasiyo tabiliwa.

Hivyo basi, swali linaloweza kuibuka ni hili: je, wimbi la matukio hayo linabeba au linatuma ujumbe gani uliojificha? Na iwapo kuna ujumbe, ni nani anautuma na kwa malengo gani?

Mfululizo wa matukio
Kabla ya uchaguzi Mkuu Oktoba 2025, kutokana na joto la kisiasa lililokuwepo, baadhi ya wadau wa siasa walishauri kufanyika kwa maridhiano ya haraka, hususan kati ya Serikali na Chadema. Mapendekezo hayo yalichochewa na msimamo wa Chadema wa kutoshiriki uchaguzi pamoja na kutosaini kanuni za uchaguzi.

Wapo walioona huo ni msimamo wa kawaida katika siasa. Hata hivyo, wachambuzi na wazoefu wengi wa masuala ya siasa waliona dalili za hatari mbele, wakitoa tahadhari na ushauri wa kutafutwa kwa suluhu ya haraka hili Chadema iweze kutengua msimamo badala yake iingie kwenye uchaguzi.

Pamoja na ushauri huo, ilionekana kana kwamba ulipewa mgongo. Wakati huohuo, baadhi ya wanachama wa Chadema waliendelea kuripotiwa kukamatwa, wengine kudaiwa kupotea, huku wengine wakiripotiwa kukimbia nchi wakitafuta hifadhi ya kisiasa.

Katika mazingira hayo hayo, Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Tundu Lissu, aliendelea kusota gerezani akikabiliwa na kesi ya uhaini. Aidha, siku chache kabla ya uchaguzi, baadhi ya viongozi wa chama hicho walikamatwa na wengine kutuhumiwa kwa makosa ya ugaidi na uchochezi. Miongoni mwa waliotajwa ni Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, John Heche, Boniface Jacob, Godbless Lema pamoja na Naibu Katibu Mkuu, Golugwa.

Baada ya kukaa mahabusu kwa siku kadhaa, viongozi hao waliachiwa huku wakipewa masharti ya kuripoti katika vituo vya polisi mara kwa mara.

Wakati matukio hayo yakiendelea, Chadema pia ilikumbwa na changamoto ya kusitishiwa ruzuku ya chama. Hatua hiyo ilifuatia malalamiko yaliyowasilishwa kwa Msajili wa Vyama vya Siasa na aliyekuwa mwanachama wa chama hicho, Lembrus Mchome. Tukio hilo lilizua mjadala mpana na mvutano wa kisiasa katika jamii hususan kupitia mitandao ya kijamii na majukwaa ya kidijtali.

Kadhalika, baadhi ya wanachama na viongozi wa chama hicho walianza kujitokeza hadharani kukikosoa chama chao katika mikutano mbalimbali na wanahabari, kabla ya kuhamia vyama vingine vya siasa hususan, Chaumma. Hata hivyo, hatua zao zilihusishwa na madai ya kuwepo kwa mkakati wa kukidhoofisha Chadema.

Pamoja na hayo, chama hicho kilikabiliwa na zuio la kufanya shughuli za kisiasa pamoja na marufuku ya kutumia rasilimali za chama. Zuio hilo lilitokana na uamuzi wa Mahakama kufuatia kesi iliyofunguliwa na aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema Zanzibar, Said Issa Mohammed.

Kesi hiyo inaendelea hadi sasa, huku zuio hilo likiripotiwa kubaki palepale. Wapo wanaoiona kesi hiyo kama sehemu ya mkakati uliosukwa kisiasa.

Kadiri siku zilivyokwenda, licha ya baadhi ya wanachama wake kutimkia Vyama vingine Chadema iliendelea kushikilia msimamo wake bila kuubadili. Hatimaye uchaguzi ukafanyika katika mazingira ambayo yaliandika sura mpya katika historia ya siasa za Tanzania. Ambapo Chama hicho kikuu cha upinzani hakikushiriki.

Katika uchaguzi huo, mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, alitangazwa mshindi wa kiti cha urais kwa kupata zaidi ya asilimia 97 ya kura, na baadaye kuapishwa rasmi kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Baada ya kuapishwa kwake, viongozi wa Chadema wameendelea kueleza wazi kutoutambua uchaguzi huo pamoja na matokeo yake. Kwa mujibu wao, mchakato mzima wa uchaguzi pamoja na matokeo yake haukuwa halali. Msimamo huo umeendelea kusisitizwa katika kauli zao za mara kwa mara.

Katika mazingira hayo ya sintofahamu ya kisiasa, wachambuzi mbalimbali walitabiri uwezekano wa kufanyika kwa maridhiano ya haraka baada ya uchaguzi. Mtazamo huo ulijengwa juu ya hali ya kisiasa na kijamii iliyokuwepo wakati wa uchaguzi na baada yake.

Wengi walitabiri kuwa “nati” iliyokazwa dhidi ya Chadema ingeanza kulegezwa ili kubadili upepo wa kisiasa ili kujenga uwepesi wa maridhiano. Ambapo wengi waliona hatua hizo zingejumuisha kuondolewa kwa baadhi ya kesi zenye harufu ya kisiasa ikiwemo kumuachia huru Tundu Lissu pamoja na kuondoa kesi ya mgawanyo wa mali iliyopelekea zuio la shughuli za kisiasa na kuwaachia baadhi ya wanachama wanaodaiwa kushikiliwa.

Hata hivyo, hadi sasa zaidi ya siku 100 zimepita tangu Serikali mpya chini ya Rais Samia Suluhu Hassan irejee madarakani. Kinyume na matarajio ya wengi, hali imeendelea kuwa tofauti, huku Chadema ikiendelea kupitia kipindi kigumu chenye misukosuko ya kisiasa, jambo linaloweza kuwa linaongeza wingu kwenye siasa za Tanzania.

Mwenyekiti wa chama hicho bado yuko gerezani akikabiliwa na kesi ya uhaini. Wakati huo huo, zuio la shughuli za kisiasa bado linaendelea. Ambapo imefikia hatua ambapo fursa pekee ya viongozi na wanachama wa Chadema kukutana imebaki kuwa katika viunga vya Mahakama Kuu wakati kesi ya Lissu inapokuwa ikisikilizwa.

Hapa ndipo swali linapoibuka:Kibano hiki kina ujumbe gani?
Kama ilivyoelezwa awali, katika siasa kila tukio huwa na kusudio. Je, hali ya misukosuko inayoikabili Chadema inabeba ujumbe gani?

Yasemwayo
Kwa nyakati tofauti kumekuwepo na madai katika mitandao ya kijamii kuhusu uwezekano wa kukifuta chama hicho. Je, huo ndio ujumbe unaotumwa? Na kama ndivyo, unatoka kwa nani? Kwa maslahi ya nini?

Baada ya uchaguzi kumalizika, kulikuwa pia na utabiri au ahadi za kuwepo kwa maridhiano. Hata hivyo, hadi sasa Chadema haijaonyesha utayari wa wazi kushiriki mchakato huo, ikiendelea kushikilia misimamo yake ya awali. Je, kibano kinachoendelea kina lengo lolote la kulazimisha kulegezwa kwa msimamo huo? Na ni nani anayeratibu mkakati huo?

Pia kumekuwepo na madai kwamba kiongozi mkuu wa chama hicho amekuwa mgumu kukubali masharti ya maridhiano pamoja na kubadili misimamo yake ya kisiasa. Je, inawezekana bahasha hii ya misukosuko imebeba ujumbe wa kumshawishi abadili msimamo?

Wapo pia wanaohusisha hali ya sasa na yaliyotokea katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, hasa msimamo wa Chadema wa “No Reform, No Election.” Je, kibano kinachoendelea ni aina ya adhabu au kulipiza kisasi cha kisiasa, kama baadhi ya madai yanavyodokeza?

Wahenga walisema, “kila jambo lenye mwanzo halikosi mwisho.” Katikati ya hali hii ya sintofahamu, wengi wanabaki na hamu ya kujua ujumbe gani hasa umebebwa ndani ya bahasha hii ya misukosuko ya kisiasa? Je, utatimia?

Swali linaloacha tafakari
Je, Chadema wameshang’amua ujumbe uliopo ndani ya bahasha hiyo? Kama ni mkakati, wahusika wamepima maslahi ya Taifa kwenye mkakati wa kufikia kusudio lao?
 
kilicho nyuma ya hicho chama useless,
ni uropokaji nonsense wa viongozi wake wa kitaifa hususani kibaraka wa mabwenyenye ya magahribi na mamluki wake malofa na wasio na maono na waliopoteza uelekeo.
 
si mna Mahakama, na Majaji si ni wenu! Mleteni basi AJE AWAGARAGAZE na vikesi vyenu!
 
calm down,
hakuna kibaraka atakaefurukuta na nonsense zake Tanzania,
watu wa aina hiyo makazi yao mwisho ni jela tu maisha yao yote gentleman
 
kilicho nyuma ya hicho chama useless,
ni uropokaji nonsense wa viongozi wake wa kitaifa hususani kibaraka wa mabwenyenye ya magahribi na mamluki wake malofa na wasio na maono na waliopoteza uelekeo.
Useless ni mamako aliyekuzaa wewe useless na mabwabwa wenzio huko ccm mnaokesha kuimba mapambio useless ya kumsifu muuwaji nguruwe wa lumumba nyinyi
 
calm down,
hakuna kibaraka atakaefurukuta na nonsense zake Tanzania,
watu wa aina hiyo makazi yao mwisho ni jela tu maisha yao yote gentleman
Mabwabwa ya Abdul lazima mpate dementia na depression nguruwe mnaofugwa kwenye makorido ya Lumumba na huyo kiongoz wenu fake.
 
Back
Top Bottom