Nini kisababishacho hili

Nimeanza kuelewa somo sasa kwa bahati mbaya Sina kazi za kutumia nguvu, ila kuongea kwa sana tu
Maji mengi yanahitajika mwilini kwa ajili ya metabolic activities.

Kwa hiyo unapokunywa maji , hayo maji yanafyonzwa yanapofika kwenye loop of Henle ili yakafanye kazi yake mwilini , reactions nyingi mwilini zinafanyika kwa kutegemea maji, ubongo unafanya kazi take vizuri kwa kutegemea maji, bonds nyingi ili zivunjike zinategemea uwepo wa maji nk.

Kwa hiyo ukinywa maji ya kutosha (excess water) mengi yatafyonzwa mwilini na mengine ambayo hayahitajiki yatatolewa nje kupitia njia ya mkojo.
 
Sawa mkuu na ni nini kisababishacho pale ambapo nitakua nimetumia maji kiasi hichohicho cha kila siku na kutumia Lasix huwa unakua mweupe sa kunauhusiano gani hapo.,?
Mkojo kuwa mweupe kuna tegemea pia na hali ya hewa.

Kama hali ya hewa ni ya ubaridi ina maanisha kuwa the rate of dehydration itakuwa ni ndogo sana kwa hiyo kwa hiyo kiasi kidogo sana cha maji kitafyonzwa mwilini na mengi yatatolewa nje kwa njia ya mkojo kwa kuwa vinyweleo vya kutolea jasho vinakuwa vimeziba.
 
Mkojo wa njano nikawaida....
Ukikosa maji mwilini unabadilika kwenda njano chafu au kahawia.

Jiangalie chakula unachokula au kama kuna vidonge/dawa unatumia inaweza sababisha rangi ya mkojo kubadilika.

Ili uwe na amani kapime mkojo kwenye maabara zinazoaminika ujue huna tatizo na endelea kunywa maji kwa wingi, ila usizidishe maana nalo nitatizo.
 
Ahsante mkuu nabidi ni Ongeza kiwango cha unywaji wa maji toka Lita nne mpka sita walau hata kwa wiki moja nione kama nitafanikiwa
 
Ahsante mkuu nabidi ni Ongeza kiwango cha unywaji wa maji toka Lita nne mpka sita walau hata kwa wiki moja nione kama nitafanikiwa
Anza hata kesho halafu ulete mrejesho uone kama utaendelea kukojoa mkojo wa njano (Concentrated Urine)au lah.
 
Sawa mkuu na ni nini kisababishacho pale ambapo nitakua nimetumia maji kiasi hichohicho cha kila siku na kutumia Lasix huwa unakua mweupe sa kunauhusiano gani hapo.,?
Laxis unatumia kwa maagizo ya Daktari?
 
Ahsante kwa ufafanuzi na ushauri kupima napima but majibu huwa hakuna shida, swala LA maji ni muhimu kutumia kiasi gani kwa siku.?
 
Wakati wa joto mwili unapoteza maji mengi kwa njia ya jasho.Hivyo figo zinatengeza kiasi kidogo cha mkojo ili kuhifadhi maji mwili usikauke.Na uchafu wote wa mwili unaweka katika kiasi hiki kidogo cha mkojo ndio maana mkojo unakuwa wa njano sana.

Wakati wa baridi mwili haupotezi maji mengi kwa njia ya jasho.
 
Ahsante kwa ufafanuzi na ushauri kupima napima but majibu huwa hakuna shida, swala LA maji ni muhimu kutumia kiasi gani kwa siku.?
Unapaswa kunywa si chini ya lita 3 kwa siku. ...ingawa inategemea na hali ya hewa ya mahali ulipo na kazi ufanyayo.
 
Unapaswa kunywa si chini ya lita 3 kwa siku. ...ingawa inategemea na hali ya hewa ya mahali ulipo na kazi ufanyayo.
Ahsante kwa hilo mkuu mie hupitiliza Lita tatu kwa siku
 
Yeah ni dawa ambayo nahitumiaga
Fuata maagizo ya Daktari aliyekuandikia laxis...kujua ni kiasi gani cha maji unatakiwa kunywa.
All in all unahitaji kunywa maji mengi kuzua kukaukiwa, mpaka hapo utakuwa unajua kazi ya laxis mwilini.

Mwanzoni ungesema unatumia laxis ungeweza kushauri vizuri zaidi kulingana na tatizo linalokufanya utumie laxis.
 
Yeah najua kazi yake ila before Sina Anza kutumia dawa hiyo shida hiyo ilikuwepo ila baada ya siku ambayo nilipewa Lasix ndipo niliona nikikojoa mkojo unakua mweupe but kwa siku moja tu siku nyingine ni kulekule kwa njano
 
Mrudie Daktari mueleze, maana hapa ni ngumu kukupatia jibu bila kujua tatizo lako linalokufanya utumie laxis.
Ondoa hofu mkuu, endelea kunywa maji kwa afya, matatizo yanarekebishika.
 
Mrudie Daktari mueleze, maana hapa ni ngumu kukupatia jibu bila kujua tatizo lako linalokufanya utumie laxis.
Ondoa hofu mkuu, endelea kunywa maji kwa afya, matatizo yanarekebishika.
Ahsante mkuu kwa ushauri wako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…