JUICE ...JUSI/JUISI (yoyote kati ya hayo ni sahihi)
COCKTAIL ... mchapalo
DIGITAL .... kidijito (kuna mjumbe alisema dijito...hapana; maana kuna kiambishi katika neno 'digital' kwa hiyo tunashukuru kw akutukumbusha kuwa tusiseme 'dijitali' bali tuseme dijiti. hata hivyo naomba kurekebisha ni KIDIJITI
Decoder... nakubaliana na mjumbe kuwa ni kisimbuzi na sio king'amuzi (maana kusema kweli tukikiita ;king'amuzi' ina maana kina utashi wa kung'amua??)
Asante tuendeleeni kusaidia kurekebisha makosa ya hapa na pale kuhusu lugha yetu. kwani Tanzania na Watanzania ndio kioo duniani/ulimwenguni katika Kiswahili...kama huamini hebu sikiliza Kiswahili cha wenzetu Wakenya...Wakongo...nk.
Lakini jamani inafikia wakati tukubali kuwa Kiswahili kimekopa maneno mengi sana tu kutoka kwenye lugha mbalimbali ukiacha kiarabu na kibantu!! Wengi tunafikiri neno shule ni la kiswahili kumbe tumelicopy kutoka kwa wajerumani/wareno sina uhakika (vizuri).
Naona BAKITA wakubali tu hili kuliko kutuchanganya mara DIJITI=Digital, Keyboard=Kibao mbonyezo mimi naona hii ni longo longo tu.
sasa,miwa nayo hukamuliwa na kutoa juice(juice ya miwa),na miwa sio matunda. Pia,kongosho huzalisha majimaji ambayo huitwa juice ya kongosho(pancreatic juice).ingawa ya pili haitumiki kama kinywaji. Hapo utasemaje?
cc
Kishanda,
MadameX,
Queen kan,
Mjepu.