Mmh watu hupigana wakitafuta amani mbona sio kweli, kwani kupigana huja mnapokubaliana au kutofautiana?. Penye amani ndo Penye mafanikio, penye maisha. Amani huzaa haki, na haki huendana na wajibu.
Unapiganaje kutafuta amani wakati kupigana kwenyewe huondoa amani?!
Na hata kama ingekuwa watu wanapigana kutafuta amani, bado pia ulitakiwa kutafuta kwanini walipigana!!
Watu wanapohangaika kutafuta amani kwanza ndipo haki ichukue nafasi ni katika mazingira ambayo tayari amani imeshavurugika, na katika mazingira kama hayo, of course, no peace no justice!!!
Lakini katika nchi kama yetu tunatakiwa kutafuta na kutoa haki kwanza ili tusifikie kupigana kutafuta haki na hatimae kulazimika kutafuta amani kwanza ndipo haki itawale!!
Mababu zetu walipigana Vita Vya Majimaji sio kwa ajili ya kutafuta amani bali kutafuta haki ambayo ilipokonywa na Wajerumani na kuwafanya babu zetu kama viumbe dhalili!!
Kule Nigeria kulitokea vita vya wenyewe kwa wenyewe in the name of Biafra War! Watu wa Biafra hawakuanzisha vita ile kutafuta amani bali walianzisha kupigania kile walichoona kukiukwa kwa haki zao!!!
Enzi za ubaguzi wa rangi kule SA vurugu zilikuwa haziishi!!
Vurugu zile za SA hazikuwa za kutafuta amani bali za kutafuta hakl ambayo iliporwa na makabaru na kuwafanya watu weusi kuwa ni watu wa daraja la chini!!
USA nako kumekuwa zikitokea vurugu! Vurugu zile zinatokana na kile kinachodhaniwa mamlaka kutotenda haki kwa watu weusi na wala sio vurugu za kutafuta amani!!!
Watu wa CCM wamekuwa wakiwaita wale wale wanaowasaidia kwa majina mabaya kama vile Mabeberu! Hasira hizi za wana-CCM bila kujali kama zina mantiki au hapana hazitokani na wao kuamini kwamba Mabeberu wanavuruga amani nchini bali zinatokana na wao kuamini Mabeberu wanaingilia mambo ya ndani ya Tanzania wakati mambo ya ndani ya nchi ni haki ya kimsingi ya any sovereign state!!!
Itoshe tu kusema kwamba, more often than not, ukiona pahala amani imetoweka basi hapo kuna haki ama imeporwa au haitekelezwi!!!
Hata ndani ya nyumba, amani hutoweka pale haki baina ya wanandoa inaposigidwa... ama mwanamke kutotekeleza wajibu kama mwanamke na hivyo kumnyima mumewe haki yake kama mume, au mume kutotekeleza wajibu wake kama mume na hivyo kumnyima mkewe haki yake kama mke!!
HAKUNA AMANI PASIPO NA HAKI, na hata ikiwepo, inakuwa sio amani bai utulivu ulio chini ya mafuta ya petroli ukisubiri cheche ndogo tu ya moto petroli iripuke na utulivu na kuunguzia mbali utulivu
!!