Nini kitarajiwe kutoka Mkutano Mkuu wa Baraza la Umoja wa Mataifa?

Nini kitarajiwe kutoka Mkutano Mkuu wa Baraza la Umoja wa Mataifa?

Sam Gidori

Senior Member
Joined
Sep 7, 2020
Posts
165
Reaction score
417
Umoja wa Mataifa unatimiza miaka 75 mwaka huu; Mkutano Mkuu wa Baraza la Umoja wa Mataifa ulitakiwa kuwa mkutano mkubwa hasa kutokana na kusherehekea Jubilee hiyo ya Platinamu. Kama ilivyokuwa kwa miaka 74 iliyopita, viongozi kutoka mataifa mbalimbali duniani husafiri na kukusanyika mjini New York kwa ajili ya kushiriki tukio hilo muhimu duniani, lakini hali ni tofauti mwaka huu! Mkutano huo unafanyika kwa njia ya video, ikiwa ni sehemu ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona, huku idadi ya wajumbe watakaoruhusiwa kushiriki ikizuiwa kuwa mjumbe mmoja tu kwa nchi.​

Mkutano Mkuu wa UN 2020.jpeg

Dunia inakabiliwa na mapambano dhidi ya virusi vya corona, na suala hilo litakuwa ajenda muhimu ya mkutano wa mwaka huu. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterez hakusita kuonesha tofauti ya mkutano wa mwaka huu na mikutano mingine.​

"Tutafanya mikutano kadhaa kwa njia ya video kuhusu masuala muhimu yatakayotugusa, lakini hatutakuwa na ule ukaribu wa kukutana uso kwa uso ambao, ninaamini, una maana kubwa sana katika kuifanya diplomasia kuwa na maana," alisema Guterez.​

Tutegemee nini kutokana na mkutano huo?
Mkutano Mkuu wa mwaka huu utashuhudia zaidi ya hotuba 170 kutoka kwa viongozi mbalimbali duniani zitakazooneshwa kwa njia ya video. Mkutano huu huangazia masuala muhimu ya kidunia ikiwamo masuala ya usalama, haki za binadamu na mabadiliko ya tabia ya nchi, lakini suala la mlipuko wa virusi vya corona linatarajiwa kutawala mazungumzo katika mkutano wa mwaka huu, hasa kutokana na tofauti ya kimtazamo na kiutendaji kutoka mataifa mbalimbali duniani.​

Katika hotuba yake aliyoitoa siku ya Ijumaa, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani, Tedros Ghebreyesus anasisitiza viongozi mbalimbali duniani kuchukulia uzito suala la kuungana ili kufanikisha mapambano dhidi ya virusi vya corona.​

"Tatizo kubwa tunaloliona duniani kwa sasa ni kukosekana kwa umoja wa kidunia; mataifa makubwa duniani hayafanyi kazi kwa pamoja. [Mataifa hayo] yanatakiwa kufanya kazi kwa pamoja kama yataonesha nia ya dhati ya kutatua changamoto hii ya mlipuko [wa virusi vya corona]. Ni kwa kuwa na umoja thabiti," anasema Ghebreyesus.​

Mataifa hayo yanatakiwa kufanya kazi kwa pamoja kama yataonesha nia ya dhati ya kutatua changamoto hii ya mlipuko wa virusi vya corona.
- Tedros Ghebreyesus
Karibu viongozi wote wa nchi wanachama wa kudumu wa baraza la usalama la umoja wa mataifa wanatarajiwa kuzungumza hapo siku ya Jumanne: Rais wa Marekani, Donald Trump, Xi Jinping wa China, Vladimir Puttin wa Urusi, Emmanuel Macron wa Ufaransa na Hassan Rouhani wa Iran - wote wanatarajiwa kuzungumza.​

Masikio ya wengi, hata hivyo, yanasubiri atakachozungumza Rais wa Marekani, Donald Trump, ambaye anagombea kupata miaka mingine minne ya kuliongoza taifa la Marekani, kuhusu Iran, China au hata kumhusu Joe Biden.​

Tofauti nyingine inayotarajiwa kujitokeza katika mkutano wa mwaka huu ni kuhusu idadi ya watu wanaotarajiwa kutazama au kusikiliza mkutano huu wakiwa majumbani. Katika mikutano ya kawaida, idadi ya watu hupungua baada ya hotuba za viongozi wa mataifa yenye nguvu duniani kama Marekani kumalizika. Utata unaongezeka zaidi kutokana na kuwa kila mtu ana uwezo wa kujiunga na kutoka katika mkutano huu muda wowote akiwa nyumbani.​

Kama hiyo haitoshi, mkutano huu pia unatarajiwa kutawaliwa na idadi kubwa ya viongozi wa kiume, na ni hadi pale kiongozi wa 51 atakapozungumza katika orodha ya viongozi duniani, ndipo sauti ya mwanamke itakaposikika: Rais Zuzana Čaputová wa Slovakia.​

Ukumbi wa Mkutano huo unatarajiwa kuwa mkavu ukilinganisha na miaka yote. Mwanadiplomasia mmoja tu kutoka kila nchi ndiye anayetarajiwa kuiwakilisha nchi yake, kila mmoja akiwa amekaa umbali salama kutoka kwa mwenzake. Jumla ya watu 210 wanatarajiwa kuwepo katika ukumbi uliozoea kuwa na washiriki zaidi ya 2,500.​

Kila nchi inayoshiriki ilitakiwa kutuma video ya hotuba yenye urefu wa dakika 15, tofauti na miaka kadhaa ambapo hotuba ya kiongozi wa zamani wa Cuba, Fidel Castro ilidumu kwa muda wa dakika 269, ama Kanali Muammar Ghadafi, ambaye dunia ililazimika kumpisha kwa takriban dakika 100 kusikiliza hotuba yake.​

Kando ya mkutano huu, mikutano mingine inatarajiwa kufanyika kuangazia masuala mbalimbali kuanzia mabadiliko ya tabia ya nchi hadi hali ya kibinadamu nchini Lebanon.​

Chanzo: Al Jazeera, CNN
 
Hizi ndio habari P. Mayalla alikua akiziibua ila sasa kaamua kwenda kutafuna pesa za Gwajima huku akimlaghai kwa kampeni uchwara.
 
... kwa njia ya video conference Tanzania isipowakilishwa na mzee baba itakuwa maajabu maana suala la safari halipo tena suala ambalo kama anavyodai limekuwa "likimuumiza sana".
 
... kwa njia ya video conference Tanzania isipowakilishwa na mzee baba itakuwa maajabu maana suala la safari halipo tena suala ambalo kama anavyodai limekuwa "likimuumiza sana".
Le prof au Mama Samia watawakilisha.. Mimi nipo kuomba kura kwa watanzania 🤣
 
Back
Top Bottom