Nini kitatokea baada ya Magufuli kustaafu Urais?

Freed Freed

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2017
Posts
6,547
Reaction score
7,167
Habari wadau wa JF siasa.

Nimekuwa nikiwaza Sana sura ya nchi na hali ya nchi hii baada ya Rais Magufuli kumaliza mihula yake miwili. Je nchi itakuwaje kirushwa na kifisadi, kiuchumi, kisiasa, kijamii, kimaendeleo nk?

Ajaye atakuwaje na atatupeleka wapi jamii ya Kitanzania kipindi hicho kitakuwaje?
 

Kusema ukweli, we endelea kuwaza kijana wangu
 
Hatatoka
 
Ndio maana mnaambiwa jengeni mifumo badala ya personalities. Binadamu tunapita; nchi na mifumo yake hudumu.

Kwenye hili CCM mmekwama completely toka enzi za Mwalimu. Anyway, sio kwa bahati mbaya ila makusudi mazima ili muendelee kutawala kijanja janja. Ila mwisho upo.
 
1. Miradi mingi ambayo aliianzisha itasimama

2. Chattle kitabaki kijiji kama zaman tena enzi za nyerer kabisa

3. Uwanja wa chattle utakuwa eneo la kuchezea mpira na matamasha ya dini

4. Viongozi wengi wataonyesha uhslisia wa kipindi cha mzee magufuli..

Ntakuja baadae kidogo.. Naenda kwenye uzi wa kula tunda kimasihara
 
Hata anachofanya polepole kupokea matatizo ya watu kwenye simu channel ten ni utopolo mtupu jengeni mifumo imara itakayosimamia kwa haki sheria na taratibu za nchi kinyume na hapo ni sifa za kijinga mnataka kujipatia.
 
Tutaendelea kama kawaida, maana kama rushwa bado ipo, kama ufisadi bado upo sema shida ni kwamba tofauti na kipindi cha JK bunge haliwezi kuyaongelea, Tanzania imejitoa kwenye uwazi hivyo mikataba siku hizi ni siri hatutakiwi kujua yaliyomo. Vyombo vya habari vimepigwa ganzi hakuna tena ile mijadara ya wazi na uandishi chokonozi.

Utashangaa mambo yatakayoibuka baada ya jamaa kumaliza awamu yake watu wakapata uwezo wa kuanza kuongea. Wale wale waliokuwa wanampamba kikwete aendelee leo hii ndiyo wanasema awamu iliyopita ilikuwa mbovu sana. Kila zama na mfalme wake.
 
Sidhani Kama Kuna ufisadi sikuizi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…