Nini kitatokea endapo IMF & World bank zikifilisika?

Nini kitatokea endapo IMF & World bank zikifilisika?

KISIWAGA

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2015
Posts
8,022
Reaction score
16,563
Kwa wale waliosoma issue za uchumi wajaribu kunielewesha ni kipi kitatokea endapo taasisi tajwa hapo juu zitafilisika ghafla

Je, ni kipi tufanye sisi raia wa kawaida kujiandaa na matokeo ya kufilisika kwa mashirika tajwa hapo juu.

Halafu je mpaka sasa korona hajaweza kuzitia misukosuko ya kifedha taasisi hizi za mabeberu.
 
Hawawezi filisika kamwe, sababu chanjo ni endelevu. Ya kwanza bure za kuendelea na pesa, wanaita booster!
Mkuu naona kama wanakopesha mno au kuna namna wanapata sapoti kutoka kwa mashetani bill gates na wenzake wanaoipigia chapuo depopulation
 
Hizo ni taasisi ambazo hazipo kibiashara (sio kwa ajili ya faida) hivyo swala la kufilisika hamana. labda tu useme nchi zinazowapa bajeti za kujiendesha zikiacha apo ndo itakua mwisho wao. Ni kama tu BOT huwezi sema itafilisika au itapata faida ama hasara kwa sababu hayo sio malengo yake. malengo hua ni utekelezaji wa sera za fedha na uchumi kwa ujumla wake.
 
Tutakulaje mihogo,unakula mihogo mpk ukifumba mambo unaona maandishi mekundu yakiwa yamejiandika hivi "HATA KAMA!"..😂
 
Kufilisika kwa IMF na World bank kwisha kwa rasilimali za afrika na mafuta ya Middle East. Nao ndio watafilisika


Lunatic [emoji2957][emoji2957][emoji2957]
 
Kwa wale waliosoma issue za uchumi wajaribu kunielewesha ni kipi kitatokea endapo taasisi tajwa hapo juu zitafilisika ghafla

Je, ni kipi tufanye sisi raia wa kawaida kujiandaa na matokeo ya kufilisika kwa mashirika tajwa hapo juu

Halafu je mpaka sasa korona hajaweza kuzitia misukosuko ya kifedha taasisi hizi za mabeberu
Hii ni future impossible tense..
 
Hawawezi wana reserve kubwa mnoo ya vito vya thamani na madini waliyotuibia kwa bei chee mno.. Na wamewekeza kwenye biashara kubwa kubwa duniani... Halafu wanaidai dunia mabilioni ya dola
Sasa ilikuaje yule jamaa kituko wa chattle kuwavimbishia kifua chake chenye betri kwa miaka mitano
 
Mi naogopa sana watu wenye maono kama haya maana mtu humjui wala hujui katoa wapi wazo hilo, kumkatalia kwamba haiwezekani naona kama sio sawa(hatumtendei haki) . Humu JF kuna watu wanaona mbali na maono yao tumeyathibitisha wakati awali tulikataa maono hayo, mfano watu walitabiri magufuli angekuwa raisi 2015 wengi tulibisha ila ikawa, wengine walitabiri tutapata raisi kutokea kwenye makamu, tukabisha ikawa, wengine wakatabiri tutapata raisi mwanamke hivi karibuni, tukabisha imekuwa, mi naomba wataalamu (bahati mbaya mimi sio) wajibu hili swali itakuwaje wakifilisika, hayo mengine ya kuwezekana au kutokuwezekana tumuachie Mungu.
 
Kwanza, World Bank inapata pesa Kwa njia ya michango unaofuata muundo wa shareholders.

Shareholder mkubwa wa WB ni Marekani mwenye share za 16.66%.
Juma ya nchi nane zinachangia 45.61%, hao ndio waidhinishaji WA mikopo kwenda Kwa nchi zinazoomba mikopo na USA akikataa basi nchi husika haipati mkopo.

Kwa WB kufirisika inaweza tokea endapo wachangiaji wakubwa (nchi 8) wasitishe kutoka funds zao.

Mbadala WA World Bank ni Brics endapo WB itapangalanyika.

Umoja WA Brics unahusisha nchi za Brazil, Russia, India, China na South Africa.
Wamejipambanua kuwa tofauti na wb katika utowaji WA mikopo Kwa nchi masikini.

Mpaka sasa Brics haijaweza kuikaribia WB.
WB na IMF zinaweza Kufa pale USA ikianguka.

USA ndio mwanzilishi na zipo Kwa ajili ku-accomodate ushawishi wa Marekani duniani.
 
Back
Top Bottom