Ni imani tu, ila mwanadamu akishakufa kumbukumbu lake linatoweka hawezi jua kinachoendelea duniani....soma Ayubu hapa chini.
AYUBU: MLANGO 14.
10 Lakini mwanadamu hufa, huifariki dunia; Naam, mwanadamu hutoa roho, naye yupo wapi?
11 Kama vile maji kupwa katika bahari, Na mto kupunguka na kukatika;
12 Ni vivyo mwanadamu hulala chini, asiinuke; Hata wakati wa mbingu kutokuwako tena, hawataamka, Wala kuamshwa usingizini.
21 Wanawe hufikilia heshima, wala yeye hajui; Kisha wao huaibishwa, lakini yeye hana habari zao.
Kwa hiyo utaona kwamba waabudu mizimu, wakiwemo wale watambikaji huwa wanaishia kuabudu mapepo tu, maana marehemu hawajui lolote linaloendelea katika nchi ya walio hai.