Nini kitatokea ikiwa wananchi watakuwa na msonono na kutoufurahia uchaguzi wa 2025?

Nini kitatokea ikiwa wananchi watakuwa na msonono na kutoufurahia uchaguzi wa 2025?

Mikopo Consultant

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2024
Posts
2,375
Reaction score
4,784
Tukiwa tunazielekea siku sitini (60) kabla ya tarehe 27 Octoba - inayotajwa kuwa ya uchaguzi; bado huku mitaani na vijijini watu hawaujadili uchaguzi; ikimaanisha kwa jicho la uchambuzi kwamba: kuna hali ya kuendelea kwa msonono miongoni mwa wananchi tunapoikaribia hiyo tarehe, tofauti kabisa na chaguzi za 2015 na 2020.

Nahisi kuna matukio mengi ambayo CCM wameyatekeleza ama wanayatekeleza, ili kuwachechemua wananchi wengi waujadili na wautamani uchaguzi. Ukiachilia ile gala dina ya mabilionea wa taifa; kuna hii chombeza ya Humphrey Polepole na Mchungaji Gwajima ambayo bado inaendelea (naiita chombeza kwasababu naona ni sarakasi za kuwachechemua wananchi).

Lakini kinachonishangaza, mbinu zote hizi, hazijaweza kutengeneza momentum ya kudumu kwa wananchi - yanawapandisha wananchi moto kuhusu uchaguzi lakini baada ya muda mchache, tempo yote inarudi ground zero. Hii kwangu naitafsiri kwamba: hii hali ya kusonona bado ina nguvu kuzidi mchechemuo wowote kuhusu uchaguzi, na ndio inazaa hali ya wananchi kutoujadili uchaguzi.

Nini kitatokea ikiwa wananchi watakuwa na msonono na kutoufurahia uchaguzi wa 2025?

Watu wakiwa na sonona na wasipoufurahia uchaguzi, itasababisha raia wengi kutoheshimu na kutii mamlaka ya taasisi ya Raisi na Bunge, hivyo kutweza kwa maneno na vitendo chechefu na vya kuudhi mamlaka. Na kwakuwa sonona ipo kwa wananchi wengi, tutegemee sura mpya zaidi za wanaharakati wenye maneno na matendo ya kutweza mamlaka.

Haya yakitokea: maana yake ni kwamba, kunaweza kuwa na hatari ya mwaka 2026, kugeuka kuwa ni ambao utakithiriwa na vitendo vile vile vya utekaji na mauaji, kwasababu zile zile zilizoonekana kipindi cha nyuma - cha wale watwezao taasisi ya Urais, kuwa wahanga.

Je, hii hali inaweza kudhibitika?

Kudhibiti hii hali maana yake ni endapo kutatokea nguvu ya kuondoa sonona hii iliyopo kwa wananchi na kuwafanya waujadili na wautamani uchaguzi, na njia pekee ilikuwa ni Tundu Lisu kupatiwa haki yake (apewe mastahili yake kwa mujibu wa sheria), lakini pia, zoezi hili lingepaswa kwenda sambamba kabisa na ikiwa CHADEMA ingeshiriki uchaguzi 2025. (Ili kuwepo na amani 2026, ingelibidi hayo mambo mawili yatokee sambamba kuelekea uchaguzi wa 2025)

Kwakuwa hayo mambo mawili ni magumu kutekelezeka kwa namna mambo yanavyokwenda; ni vema CCM na serikali kujiandaa na matokeo wasiyoyapenda.

Ni utabiri tu!
MC
 
Back
Top Bottom