Nini Maana Na Tofauti ya Akili, Nafsi na Roho?

Mchanya

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2015
Posts
997
Reaction score
1,568
Naomba msaada kwa mwenye uelewa anisaidie (Kwa lugha rahisi) kuelezea maana na tofauti ya maneno haya (Akili, Nafsi na Roho). Ikiwezekana kwa mifano halisi au kama kuna vitabu au tovuti ambayo inaweza kuelezea kwa kina dhana hizi za Akili, Nafsi na Roho. Nimeyasikia maneno haya mara kadhaa nahisi wakati mwingine nayachanganya kwenye kuelewa na matumizi yake. Pia kama naweza kupata tafsiri yake kwa Kiingereza nitashukuru sana kwa msaada wenu.

Mbarikiwe sana
 
Hivi vitu nilijifunza bible study.
Roho imebeba Nafsi, na akili hukaa katika nafsi.

KitU hadi kiwe imani ndani ya roho yako, lazima kipite kwenye akili zako kwanza, akili yako ikubaliane na hilo jambo ndipo itajengeka imani hili ni kwa wale tuaminio kwa roho na kweli.

Kama ni msomaji wa Bible wameelezea
 
Naomba msaada kwa mwenye uelewa anisaidie (Kwa lugha rahisi) kuelezea maana na tofauti ya maneno haya (Akili, Nafsi na Roho). Ikiwezekana kwa mifano halisi au kama kuna vitabu au tovuti ambayo inaweza kuelezea kwa kina dhana hizi za Akili, Nafsi na Roho. Nimeyasikia maneno haya mara kadhaa nahisi wakati mwingine nayachanganya kwenye kuelewa na matumizi yake. Pia kama naweza kupata tafsiri yake kwa Kiingereza nitashukuru sana kwa msaada wenu.

Mbarikiwe sana
Akili ni uwezo wa ubongo wako kufanya kazi. Kama akili yako ina ubora wa juu utakua unafanya maamuzi yenye tija kila wakati.
Nafsi yako ni wewe mwenyewe mwili na akili yako. Yaani mawazo unachoamini unachosema.
Roho inaishi ndani ya mwili ni sehemu ya nafsi yako. Ni ule uhai na kujitambua ambao kwenye dini wanaamini ukifa mwili roho haifi inaenda mbele ya mwenyezi mungu kwa hukumu.
Ukweli wa kisayansi roho inaishi ndani ya mwili wa binadamu. Ni kule kujitambua ambao viumbe wengine hawana. Kisayansi ukifa roho yako nayo inakufa kwa sababu haiwezi kuishi nje ya mwili wako na ndio mwisho wako. Kama kabla ya kuzaliwa hukuepo duniani ukifa kisayansi unakua haupo kama kabla hujazaliwa.
Ukizaliwa hujitambui kama wanyama wengine. Polepole akili yako tofauti na wanyama inakua haraka hadi unakua na ufahamu na kujitambua. Unapata nafsi.
 
kwa kifupi safari ya maisha ya mwadamu imetokea mbali sana, yaani zamani sana na katika safari hii mambo mengi yamezaliwa njiani ikiwemo imani na sayansi.

kabla ya uvumbuzi wa kisayansi wa kutambua mfumo wa ufahamu wa mwadamu tayari watu wa imani walikuwa wabaini ndani ya mwili wa mwanadamu kulikuwa na kitu kinachomuongoza mwanadamu katika kutenda.

watu wa kale walikiita kitu hicho roho ikijumuishwa katika kundi lililoitwa "incorporeal"

incorporeal lilikuwa ni kundi la vitu vilivyosadikiwa kutokuwa na physical presence yaani havina mwili ambalo lilijumuisha upepo, moto, roho n.k

lakini kadiri wanasayansi walivyopiga hatua katika kuvumbua maarifa mbalimbali, mambo mengi yaliyokuwa yakidhaniwa kutokuwa na physical presence yalifahamika vizuri kwa wanadamu ikiwemo upepo na moto.

Sasa kwa upande wa roho, roho ni layman's language ya mfumo wa ufahamu wa viumbe hai.

huu mfumo wa ufahamu ndiyo unaocontrol miili ya wanadamu.

kwa hiyo roho ni mfumo wa ufahamu wa mwadamu na akili ni kipimo cha uwezo wa mfumo wa ufahamu.
 
Naomba msaada kwa mwenye uelewa anisaidie (Kwa lugha rahisi) kuelezea maana na tofauti ya maneno haya (Akili, Nafsi na Roho). Ikiwezekana kwa mifano halisi au kama kuna vitabu au tovuti ambayo inaweza kuelezea kwa kina dhana hizi za Akili, Nafsi na Roho. Nimeyasikia maneno haya mara kadhaa nahisi wakati mwingine nayachanganya kwenye kuelewa na matumizi yake. Pia kama naweza kupata tafsiri yake kwa Kiingereza nitashukuru sana kwa msaada wenu.

Mbarikiwe sana
Akili ndio nafsi.
 
Akili ni uwezo wa ubongo wako kufanya kazi. Kama akili yako ina ubora wa juu utakua unafanya maamuzi yenye tija kila wakati.
Nafsi yako ni wewe mwenyewe mwili na akili yako. Yaani mawazo unachoamini unachosema.
Roho inaishi ndani ya mwili ni sehemu ya nafsi yako. Ni ule uhai na kujitambua ambao kwenye dini wanaamini ukifa mwili roho haifi inaenda mbele ya mwenyezi mungu kwa hukumu.
Ukweli wa kisayansi roho inaishi ndani ya mwili wa binadamu. Ni kule kujitambua ambao viumbe wengine hawana. Kisayansi ukifa roho yako nayo inakufa kwa sababu haiwezi kuishi nje ya mwili wako na ndio mwisho wako. Kama kabla ya kuzaliwa hukuepo duniani ukifa kisayansi unakua haupo kama kabla hujazaliwa.
Ukizaliwa hujitambui kama wanyama wengine. Polepole akili yako tofauti na wanyama inakua haraka hadi unakua na ufahamu na kujitambua. Unapata nafsi.
Ume dadavua vzr sana mkuu
 
Ushawahi kujikuta unamchekea mtu usoni huku ndani umenuna? Au ukaliona pochi lenye fedha limemdondoka mtu huku wewe jicho likikutoka huku Kuna sauti ndani unaisikia inakwambia kuwa Hilo pochi li la kwako hata hivyo bado ukalipiga huku ukimuacha mwenye pochi akihaha kulitafuta pochi lake na asilione?
Roho katika mwili ni Kama window ndani computer. Bila ya window computer Haina kazi.
Nitarudi...
 
Back
Top Bottom