Nini maana ya coolant na inter cooler kwenye gari?

ankai

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2017
Posts
3,282
Reaction score
4,251
jamani wanajamvi habariya jioni napenda kufahamu maana ya ivyo vitu vilivyoandikwa apo juu na mimi mnawezaje kuvijua na kuvikagua mimi mwenyewe

Maana mara nyingi wajuvi wa mambo wa apa jf wanatumiaga aya maneno lakini mimi waga sielewi manake na nawezaje kuvingamua mwenyewe na nkavitunza inavyotakikana
 
Wajuvi wa mambo karibuni
 
1. coolant, kipoozea, au maji yaliyokatika mfumo wa rejeta, kazi ni kupooza injini na venginevyo

2. kuna baadhi ya magari/truck yana supachaja/turbochaja, chaja ni air-compressor, inaishinikiza hewa kutoka nje na kuisukuma moja kwa moja kwenda katika injini, hewa ikishinikizwa presha yake inapanda, joto pia linapanda, sasa apa lazima uwe na inter-cooler, kuipooza iyo hewa ili iongeze 'ufanisi' inapochomwa.
 
( Ili kuweza kuelewa hapa inabidi uwe unajua kidogo kuhusu Combustion engine. Ujue jinsi gani Hewa inatumika kusupport combustion au kuungua kwa mafuta)

Nimejaribu kuongezea kidogo kama mleta mada bado yupo njia panda.
My credit to dronedrake
 
Coolant inategeme unaikuta kwenye engine gan kwa mfano kwenye magar mengi coolant ni aina flani ya kimiminika au maji(bt sio mazuri) ambayo hutumika kuondoa joto kutoka kwenye engine

Na kunabaadhi ya engine coolant ni ile oil inayotumika kwenye lubricatio zen hiyo oil huzunguka kwenye parts mbali mbali za engine na kugain joto halaf hupita ktk heat exchanger na mara nyingi heat exchanger hizo huwa zinatumia maji
 
Na iyo INTER COOLER je
 
Mkuu gari yangu ni raum old model kaka
Ok.
Kuna mifumo mitatu inayohusika na upozaji au upunguzaji wa joto kiwenye gari.
1. Air condition
2. Radiator
3. Inter cooler
Kila mfumo una kitu unachokipooza.

Air condition
Hii hufanya kazi ya kupooza sehemu wanayokaa abiria ndani ya gari. Hii mfumo wake ni kama wa Ac ya nyumba au friji.

Radiator
Hiki ni kifaa kinachotumika kupooza maji yanayotumika kupooza injini ya gari. Ni kifaa chenye vi pipes vidogo vidogo ambapo maji huzunguka na kupulizwa na feni hayo maji yakipozwa huzunguka kwenda kupoza injini.
Yale maji yanayokaa kwenye rejeta kwa lugha ya kiingerea huitwa coolant. Mara nyingine yale maji huwekewa madini yanayotumika kupunguza boiling point ya maji na kufanya maji yapoe kwa upesi zaidi.

Intercooler
Hiki ni kifaa kinachotumika kupozea Turbo ya kwenye gari zinazotumia Turbo. Ziko za aina mbili. Kuna Turbo inayopozwa kwa kutumia maji na pia kuna Turbo zinazopozwa kwa kutumia hewa.
Turbo zinazopozwa kwa kutumia hewa hufanya kazi ya upozaji kwa kuvuta hewa ya baridi upande mmoja na hiyo hewa huzunguka kupoza Turbo. Turbo ni kifaa kinachotumika kujaza hewa kwenye enjine ya gari kwa msukumo mkubwa zaidi ya msukumo wa asili (natural aspiration based on vacuum sucking)
 
Ok asante kaka sasa kwa gari yangu naweza kujuaje maji ambayo ndo yanayoitajika niweke na siyo maji yoyote yale
 
Na nawezaje kuitunza engine ya gari yangu
 
Mfano nataka nijue aina ya oil nnayotakiwa kuweka
 
Ok asante kaka sasa kwa gari yangu naweza kujuaje maji ambayo ndo yanayoitajika niweke na siyo maji yoyote yale
Gari yako unapofungua mfuniko wa rejeta angalia kiwango cha maji. Kama kimepungua utatakiwa kuongeza. Ila kama gari bado ni mpya, kiwango cha kupungua kwa maji huwa kinakuwaga ni kidogo sana. Weka tu maji ya kawaida ya bombani ambayo hayana chumvi.
Pia gari yako haina mfumo wa Turbo, kwa hiyo mambo ya intercooler wewe hayakuhusu.
 
Acha ujinga yani kuuliza aina ya maji ndo unaniuliza kama una leseni ama hujui kama kuna aina nyingi za maji? najibu swali lako leseni ninayo
 
Acha ujinga yani kuuliza aina ya maji ndo unaniuliza kama una leseni ama hujui kama kuna aina nyingi za maji? najibu swali lako leseni ninayo
Mkuu nmeuliza coz hayo mambo huwa yanafundishwa darasani kabla ya kupata leseni...sasa kama umenambia unayo leseni napata wasiwasi hyo leseni umeipataje..
 
Mkuu nmeuliza coz hayo mambo huwa yanafundishwa darasani kabla ya kupata leseni...sasa kama umenambia unayo leseni napata wasiwasi hyo leseni umeipataje..
Kwa iyo darasani wanajua naenda kuendesha gari ya aina gani ama iyo gari itakuwa na wengine ya aina gani? Mbona watanzania tumekuwa na akili za ivi! Angalia maelezo yanayotolewa Apo juu yanaonyesha vitu ninavyoviuliza kaka
 
Asante kaka nimeelewa vizuri nashukuru kwa muda wako
 
Kwa iyo darasani wanajua naenda kuendesha gari ya aina gani ama iyo gari itakuwa na wengine ya aina gani? Mbona watanzania tumekuwa na akili za ivi! Angalia maelezo yanayotolewa Apo juu yanaonyesha vitu ninavyoviuliza kaka
Huwa wanafundisha ndiyo na aina za gari ata kama hautaendesha au miliki..mifumo mingi ya gari inafanana..ukiachana na hzo tofauti chache za kwamba hii ina turbo hii haina ..hii ina 4wheels hii ina AWD...sasa nmeshangaa ata coolant huijui..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…