Ok.
Kwenye gari kuna mifumo mitatu inayohusika na upozaji au upunguzaji wa joto kiwenye gari.
1. Air condition
2. Radiator
3. Inter cooler
Kila mfumo una kitu unachokipooza.
Air condition
Hii hufanya kazi ya kupooza sehemu wanayokaa abiria ndani ya gari. Hii mfumo wake ni kama wa Ac ya nyumba au friji.
Radiator
Hiki ni kifaa kinachotumika kupooza maji yanayotumika kupooza injini ya gari. Ni kifaa chenye vi pipes vidogo vidogo ambapo maji huzunguka na kupulizwa na feni hayo maji yakipozwa huzunguka kwenda kupoza injini.
Yale maji yanayokaa kwenye rejeta kwa lugha ya kiingerea huitwa coolant. Mara nyingine yale maji huwekewa madini yanayotumika kupunguza boiling point ya maji na kufanya maji yapoe kwa upesi zaidi.
Intercooler
Hiki ni kifaa kinachotumika kupozea Turbo ya kwenye gari zinazotumia Turbo. Ziko za aina mbili. Kuna Turbo inayopozwa kwa kutumia maji na pia kuna Turbo zinazopozwa kwa kutumia hewa.
Turbo zinazopozwa kwa kutumia hewa hufanya kazi ya upozaji kwa kuvuta hewa ya baridi upande mmoja na hiyo hewa huzunguka kupoza Turbo. Turbo ni kifaa kinachotumika kujaza hewa kwenye enjine ya gari kwa msukumo mkubwa zaidi ya msukumo wa asili (natural aspiration based on vacuum sucking)
Mjumbe nakushukuru kwa maelezo mazuri, japo ningependa kumwongezea kitu kuhusu Coolant.
1. Coolant siyo maji ya kawaida kwenye gari kama watu wengi wadhaniavyo, ni mchanganyiko wa maji fulani "deionized water" ambayo uchanganywa na aither Ethylene Graycol au wakati mwingine Glycerine na mchanganyo unatakiwa uwe 50/50. Unashauriwa usizidishe kipimo walau cha 30/70 kama umeshindwa kabisa.
-Baada yakuchanganya unaweza kutumia reflectometer kupima kama umepata mchanganyiko sawa.
2. Coolant huwa ina kitu kinaitwa freezing and boiling point, na hapa ndipo tofauti ya coolant na maji ya bomba utofautiana. Kawaida maji uchemka pale yanapopata joto la 100 degree na uganda yakifika 0, sasa coolant imeongezewa additives ambazo uipa uwezo wakuweza kuhimili joto la mpaka zaidi ya degree 100 hivyo uweza kuilinda injini isichemke, pia kwenye mazingira ya baridi coolant imepewa uwezo wa kwenda hafi kwenye negative degree na bado isigande, tofauti na maji ya kawaida ambapo yangekuwa yashaganda.
Kazi yake nini?
Kazi ya Coolant nikusafirisha joto ambalo utokana na mzunguko kwenye injini kuelekea kwenye rejeta, likishapozwa urudishwa kwenye injini kwa ajiri ya kuipoza.
Kwanini usitumie maji ya bomba?
Maji ya bomba yakipata moto yanachemka kama yakupikia ugali, yakipoa uzaa mvuke ambao ukichanganyika na hewa+chuma, baada ya muda kutu huanza kujenga ndani ya rejeta, matokeo yake njia zote uliwa na kutu, rejeta itaziba na itaanza kutoboka na kumwaga maji. Pia gari itakuwa inachemsha sana.
Kwa ufupi ukitumia coolant unazua mambo yafuatayo: freezing, boil-over, cavitation, liner pitting, erosion, corrosion, elastomer gasket degradation, na scaling.(nimekosa kiswahili but unaweza kuuagoogle moja moja).
Pitia kiambatanisho hiki kwa msaada.