Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Neno Dinozo, limetokana na jina DiNozzo ambaye ni fictional character wa kwenye tamthilia ya NCIS.menyidyo said:nini maana ya DINOZO
sure ni kweli ni dinosaur. asanteni sana.
sure ni kweli ni dinosaur. asanteni sana.
Nafikiri huyu jamaa atakuwa anamaanisha yule mnyama anaitwa dinosaur...hajapata kutokea
[TABLE="width: 926"]
[TR]
[TD="width: 540, colspan: 2, align: left"] Dinosaur wa Tanzania kurejeshwa nchini 17/07/2009
![]()
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe ametofautiana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Shamsa Mwangunga kuhusu kurudishwa nchini kwa mjusi mwenye urefu wa mita za mraba 22 (Dinosaur) aliyechukuliwa na Wajerumani mwanzoni mwa miaka ya 1900.
Wakati Waziri Membe akisema mpango wa serikali kumresha mjusi huyo nchini bado thabiti, Mwangunga alisema serikali inaangalia kama kuna uwezekano huo ama kumwacha mjusi huyo nchini Ujerumani.
Hata hivyo, Waziri Mwangunga alieleza ingawa jambo hilo bado linaangaliwa kwa makini, ni bora mjusi huyo akabaki Ujerumani kupunguza gharama za maandalizi ya kumleta na kumhifadhi nchini.
Alisema serikali inatakiwa kujenga jengo la ghorofa tatu kwa ajili ya kumhifadhi mjusi huyo aliyechukuliwa nchini enzi za ukoloni kati ya mwaka 1918 na 1919 kutoka Kijiji cha Mipingo mkoani Lindi.
Kwa mujibu wa Waziri Mwangunga, mjusi huyo anaweza kuendelea kubaki Ujerumani na Tanzania kukusanya mapato yatokanayo na mjusi huyo akiwa huko kwani gharama za kumrudisha nchini ni pamoja na kubomoa mifupa yake, kuisafirisha na kuiunda upya.
"Tunajaribu kuangalia kama kuna umuhimu wa kumrudisha mjusi huyo ama abaki Ujerumani, alisema Mwangunga akijibu swali la Mbunge wa Masasi, Raynald Mrope".
Mrope alitaka kujua sababu za serikali kuchelewa kumrudisha mjusi huyo kama ilivyoshauriwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi Elimu na Utamaduni (UNESCO) baada ya serikali ya Ujerumani kuendelea kukusanya mapato mengi kutokana na mjusi huyo.
Membe ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa alisema, uamuzi wa kurudisha mifupa ya mjusi huyo bado upo na serikali imeiandikia nchi ya Ethiopia kuomba wataalam wa kumsafirisha.
![]()
"Nchi ya Ethiopia iliunda kamati iliyofanikisha kurudisha nguzo za kihistoria nchini humo," alisema Membe akielezea wanachama wa kamati hiyo wanaweza kushirikiana na Tanzania kuona namna ya kumrudisha mjusi huyo.
Picha ya mjusi (Dinosaur) iliyotumika pichani juu, si picha halisi ya mjusi anayezungumziwa, lakini ZENJYDAR imetumia picha hiyo kama ni mfano mojawapo wa 'Dinosaur' waliokuwepo na wanaopatikana Amerika ya Kaskazini (North America), Australia na Tanzania.
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]