GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
- Thread starter
-
- #21
πππNdoto kama ikitoka kwa Mungu basi Mungu mwenyewe atakupa codes wala usijisumbue. Sababu yeye ni Top
Ukiona unaanza kutafuta tafsiri toka vyanzo vingine basi tatizo unalo wewe yaani hujatulia katika maarifa ya kumjua huyo Mungu uliyemtaja.
Siku ukiota jeneza je ?
Siumwi mkuu!Tulia dawa ikuingie mkuuπ€¨
β πππSio kweli,thus Pana watu wa kufungua codes sio wote Wana kipawa hicho
π€£π€£mambo mkuu?Siumwi mkuu!
πππNdoto yeyeyote ukiikumbuka kwa usahihi Huwa ina ujumbe
Haitakaa itokee. Mungu aliyenifanikisha Ndiye anayeyalinda mafanikio yangu..Utapitia ukata sana
Kama ni tafsiri sahihi moyo utaridhia. Kuna namna amani ya moyoni itakupa uhakika kuwa hiyo ndiyo tafsiri sahihi.sawa mkuu nimekuelewa sasa atajuaje kama tafsiri anayopewa ni ya ukweli, kuna ka mtego hapo watu wengi wanaota hela ha ha ha
πππMkuu hakuna, mwanadamu awezaye kutafsiri ndoto. Kazi hiyo no ya Mungu pekee. Soma ndoto za Yusuf na jibu la Daniel kwa Nebuchadnezzar. Hivyo hivyo, unapoota ndoto hasa za ki Mungu, Unaamshwa, tulia, Mungu mwenyewe atakupa tafsiri. Baada ya ndoto, tulia DK kadha, roho wa Mungu atakupa tafsiri. Ukiona hujapata tafsiri, basi lala, utajuwa mbele ya safari. Ndoto ni mafumbo. Huwa tunaota kulingana na mzingira ya mtu. Kwa hiyo hakuna mtu ataekupa tafsiri sahihi
Ni mapambano katika maisha yako ya kiuchumi. Inaonekana kuna riziki katika maisha yako lakini kuna watu wanataka kukudhulumu katika ulimwengu wa roho.Mimi ni Mkristo. Niaminivyo, chanzo cha ndoto inaweza ikawa:
1. Ujumbe kutoka kwa Mungu
2. Kazi ya Shetani kwa lengo la kuharibu
3. Uchovu wa mwili na aina ya mawazo uliyokuwa ukiyawaza kabla ya kulala.
Hivi karibuni, nimeota ndoto ambayo mpaka sasa bado sijapata tafsiri yake.
Niliota natembea njiani na vijana wawili, na ghafla , nikaona noti ya sh 1,000/= mbele yangu.
Nilipoiona, nilijisemea kuwa kama nimetegeshewa kichawi, basi itakuwa "imekula" kwao walioitegesha kwa sababu nitaichukua na kuitakasa kwa Jina la Yesu na kuitumia bila madhara yoyote. Niliamua kuchukua, na mara tu baada ya kuiokota, niliziona zingine nyingi, noti za shilingi 1,000/= na za 2,000/=. Niliendelea kuziokota, na nikawaambia vijana wawili niliokuwa nao kuwa na wao waokote.
Baada ya kuiokota kiasi kikubwa, ziliisha na hatimaye tukaendelea na safari kila mmoja akiwa na noti zake. Muda wote nilikuwa makini kuzishikilia huku nikiendelea kuziombea ili kama zilikuwa na nguvu za giza zisiweze kuwa na athari kwangu.
Baada ya kutembea kidogo, tuliwakuta askari watatu wa usalama barabarani wakiwa wamesimama pembezoni mwa barabara. Mmoja wao, akiwa katika sare za kazi, alinifuata na kuniambia hela tuliyoiokota ni ya kwake hivyo nimrudishie.
Kwanza, nilitaka kukataa kumpa. Lakini aliponiambia kuwa walituona tokea tulipokuwa tunaokota hizo fedha, nilipatwa na mshutuko, nikagundua kuwa huyo trafiki si binadamu wa kawaida. Aliwezaje kutuona wakati tulikookotea ni mbali?
Pale pale nilianza kumkemea kwa Jina la Yesu, na ghafla yule trafiki akaanza kubadilika kuanzia sura, umbo mpaka na mavazi.
Mavazi yake ya utrafiki (meupe) yalipoteza uweupe na kufanania kwa mbali sare za wafungwa. Na umbile la huyo askari lilibadilika kutoka wa kiume na kuwa wa kike.
Nilipoendelea kumkemea, alidondoka chini na kuwa kama anayegugumia kwa maumivu.
Vijana wawili niliokuwa nao waliondoka kwa muda na kuniacha peke yangu nikiandelea kupambana na hicho kiumbe. Ni kama vile niliwaagiza kufuata kitu.
Wakati nikiendelea kumkemea, nilimhoji sababu ya kunitegeshea pesa, akasema walinipenda. Nilipomwuliza kama hiyo hela ingewaathiri na hao vijana wawili waliookota, alisema ingewaathiri kama wangekubaliana nao.
Baada ya kusema hivyo, nilikazana kuomba kwa bidii, lengo sasa likiwa hicho kiumbe kipotee kwa kuyeyuka.
Hiyo ndoto inamaanisha nini?
Nini chanzo chake?
Asanteni.
πππzingatie sana hili
Sifi leo!Duh hy ndoto hatari sana, kuna mjomba wangu hakumaliza miezi miwili tukamwimbia tuonane paradisoΓ2
Hakuna silaha itakayofanyika juu yangu itakayofanikiwa.Kuna ukweli ndani ya hili. Atapigwa na tukio litakalomoukutisha mfuko wote kama ana vichenji chenji
Kazi ipi hy mkuu.?Sifi leo!
Sitakufa kesho!
Sitakufa keshokutwa!
Sitakufa miaka kumi yajayo!
Sitakufa miaka ishirini yajayo!
Sitakufa miaka thelathini yajayo!
Sitakufa bali nitaishi, ili niikamilishe kazi niliyoagizwa na MUNGU!
Nashukuru sana Dr. Nimepata "kitu"Nitajaribu..
Ndoto yak inaashiria mambo kadhaa muhimu:
- Jambo la kwanza Baraka na fursa Noti za shilingi 1,000/= na 2,000/= zinawakilisha baraka na fursa zinazokuja ama unazopata katika maisha yako. Ukweli kwamba uliona noti nyingi unaonyesha uwezekano mkubwa wa kufanikiwa na kupata mafanikio makubwa.Kwahyo kwenye mihangaiko yako unaweza ukapata Fursa nyingi na ukafanikiwa sana......japo bado Huamini kama mafanikio unayopata Ni ya kishirikiana au Ni ya kimungu maana yake Kuhusu Mafanikio yako bado imani yako Sio kubwa kwa Mungu
- Ulinzi wa kiroho:Kuokota noti na kuzishikilia huku ukiomba kunaashiria umuhimu wa ulinzi wa kiroho katika maisha yako. Unajua kuwa kuna nguvu za giza zinazoweza kujaribu kukuvuruga, lakini unatafuta ulinzi wa Mungu ili kuzishinda hizo nguvu za kishetani..
- Majaribu na mitego:Askari wa usalama barabarani anawakilisha majaribu na mitego inayoweza kukukwamisha katika safari yako ya maisha. Anajaribu kudai noti zako, ambazo zinaashiria baraka zako, kama njia ya kukunyima mafanikio.
- Utambuzi wa udanganyifu:Unapotambua kuwa askari si binadamu wa kawaida, unaonyesha uwezo wako wa kutambua udanganyifu na uovu. Hii ni muhimu sana katika kukabiliana na majaribu yanayokuja kwako.
- Nguvu ya imani:Kumkemea askari kwa Jina la Yesu na kumfanya abadilishe sura na umbo unaonyesha nguvu ya imani yako. Una uwezo wa kushinda maadui wa kiroho kwa kutumia imani yako kwa Mungu. Na kuwatoa kwenye nguvu walizokuwa nazo(Uanaume) na Kuwa wadhaifu (mwanamke)
- Udhaifu wa maadui:Maadui wanakupenda, lakini pia wanadhoofika na kushindwa na imani yako. Hii inaonyesha kuwa hawana uwezo wa kukudhuru kama unamwamini Mungu kikamilifu.
- Umuhimu wa ushirikiano:Vijana wawili wanaondoka kwa muda, lakini wanarudi tena. Hii inaonyesha umuhimu wa ushirikiano na msaada kutoka kwa watu wengine katika kukabiliana na majaribu. Usiache kushirikiana na watu kutatua Changamoto zako
- Ushindi: Mwishowe, unafanikiwa kumfanya yule kiumbe apotee kwa kuyeyuka. Hii inaashiria ushindi wako dhidi ya maadui wa kiroho na uwezo wako wa kufikia malengo yako.
Kwa ujumla, ndoto hii ni ishara nzuri inayoonyesha uwezo wako wa kufanikiwa maishani licha ya majaribu na mitego. Una imani yenye nguvu inayoweza kukulinda na kukusaidia kushinda maadui. Zingatia kuendelea kuomba na kuomba ulinzi wa Mungu, na ushirikiana na watu wengine wenye nia njema katika safari yako ya maisha.
uko sahihi kabisa ukijaribu kuelewa mambo ya kiroho kama hauko kiroho na ukatumia akili yako lazima uone watu wamechanganyikiwa ila time will come ambayo wale uliona wamechanganyikiwa hutapata nafasi tena ya kuwa wao. ila nafsini mwako utagundua umepoteza kitu cha dhamani sanaIbada za kwenye makanisa ya kilokole zimesha kuathiri wewe,usipojiangalia utaanza kuokota na makopo njiani.
Barikiwa sana mkuu! Asante sana.Ni mapambano katika maisha yako ya kiuchumi. Inaonekana kuna riziki katika maisha yako lakini kuna watu wanataka kukudhulumu katika ulimwengu wa roho.
Wewe pia ni kiongozi wa wengine ila itakubidi upambane sana katika roho na kila upingamizi utokao kwa mawakala wa nguvu za giza.
Unaamini katika uwezo wa nguvu ya Mungu na unajiamini kuwa kwa uwezo wa Mungu utayaweza yote. Tumia uwezo na imani hiyo vizuri kwani inakuweka katika vita ya kiroho hata kama hutambui hilo.
Ukitumia vizuri uwezo na nguvu za Mungu ndani yako utashinda.
Kuwasaidia wengine kama alivyowatumia wengine kunisaidia.Kazi ipi hy mkuu.?
Mimi na kubeti ni kama mafuta na maji.Kama unabeti, hizo ndoto ni za kawaida