Mdau Nimechafukwa, maelezo yako yana kasoro. Kila kamapuni iliyosajiliwa rasmi (hata kama ni ya kuuza vitunguu reja reja) inakuwa na hisa. Isipokuwa kuna haina mbili za kampuni. Kuna kampuni binafisi (private company) na kampuni ya umma (public company). Kampuni binafsi ni zile ambazo hazikuorodheshwa kwenye soko lolote la hisa. Kisheria (kwa Sheria ya Makampuni ya Tanzania) hizi zanatakiwa ziwe na wamiliki (wanahisa) kati ya wawili (2) mpaka hamsini (50). Kampuni ya umma, kwa upande mwingine, lazima iwe imeorodhesha hisa zake katika soko la hisa. Kwa hapa Tanzania tunalo soko moja (Dar es Salaam Stock Exchange - DSE). Kampuni ya umma haina kikomo cha wamiliki (wanahisa) bali kuna masharti mengi yanayoongoza uendeshwaji wake kuliko kampuni binafsi. Hata wewe ukitaka kuanzisha kampuni ya kuuza maandazi unaweza. Mtafute mtaalamu akutengenezee hati inayoitwa "Memorandum and Articles of Association" halafu uipeleke BRELA (Business Registration and Licensing Agency). Baada ya kutimiza masharti fulani fulani na kulipa ada ya usajili utakuwa na kampuni ambayo wewe na watu wa familia yako au washirika wako mtakuwa ndiyo wenye hisa. Haya ni maelezo ya jumla. Ni somo pana mno kulieleza kinagaubaga hapa.