Njilembera
JF-Expert Member
- May 10, 2008
- 1,496
- 609
Wana JF, Mimi Nina asili ya Bara, na maneno yanayotamkwa Kwa mkazo na hasa yenye kuanzia herufi 'ku' zinanipa hisia kuwa ni aina Fulani ya kutukana.
kwenye matangazo ya biashara ya Tigo Facebook, ninapata shida sana ninapomsikia Yule Mzee akadakia neno 'kudadeki', linaonekana ni neno baya, tusi walau Kwa matamshi. Hisia hizi zimeimarika zaidi pale ninapohusisha maneno ya utangulizi wa Yule Babu, kwamba uzee mwisho ni Msata, mijini ni ' honey' ambayo yanamaanisha uhusiano wa watu wazi a na jinsi a nyingine.
Ningefurahi kuondolewa wasiwasi huu! Je lakini, hakuna laughs nyingine ambayo ingefikisha Ujumbe huo huo?
kudadadek ni maneno yasiyo na maana mfano wake ni afanalek shabbash ni mfano ha gash(kiingereza) hayana maana ila hupata maana kihsi pind mtu anapotamka akiwa katika hali gani kuelezea hisia zake kuwa amefikia kiwango cha mwisho mfano umemuudhi au ameona kitu kilicho mvutia eg kito dem mkali au gari nyumba nk ingawa mda mwingne hutumika kama vionjo
Hakika mkuu Skype kwanza nikupongeze kwa ujasiri wa kutamka hayo maneno....na nibakie tu kuona muendelezo wa mada jadiliwa.
Ukweli ni kwamba haya maneno ni matus mfano;kumamake,kudadadeki.Kama utakuwa na ulewa fulani utaweza kupata kirefu cha neno "kumamake'',chukua japo dakika 3 ufikirie utapata jibu.
JITABOY mambo vipi mkuu? Unaizungumziaje na hii kauli hapa chini?:
Masalakulangwa ni mshenzi wa Hesabu kinyama.
neno mshenzi tayari lina maana tofaut na kudadeki ambalo naweza sema ni neno la kufikirika.
mfano wa maneno yenye maana kama huyu kijana ni nyoko usimchezee katika mambo flani maneno tayari yana maana ila watumiaji wa lugha huweza kuyatumia maneno hayo na wakelewana vile wanavyotaka wao waelewane ila huo sio usahihi wake.
ndio maana lugha hz kuepusha mgongano wa kimaana huzungumzwa tu. kwa rika au kundi la watu fulani ambao wamekubali kuelewana.
siku hizi, mtu anatukanwa ndo anasifiwa wazungumzaji hupendezewa na mdundo wa sauti (tone of the voice) na mambo yakaenda