Ina maana nyingi kulingana na makuzi yako na utamaduni wa jamii inayokuzunguka
Ila tukiziungumzia mazingira yetu ya kitanzania, ni kama kushirikiana na jamii, kupractice maadili ya jamii kama vile kuheshimu wakubwa, kusaidia wazee, kuheshimu wazazi, kushiriki mambo ya kijamii kama misiba, sherehe nk kama unaishi mjini basi siku ukienda kijijini hakikidha unapita kwaaa majirani na ndugu kuwasalimu hata na kilo moja ya sukari, anapotokea mgonjwa katika jamii unayoishi unatenga muda hata wa kutoa pole, anapotokea mzazi kwente jamii unayoishi basi unatoa hongera na mambo kama hayo
Kwa kifupi maisha ya kiafrika ni magumu sana its all about satsifying people hata kama huna uwezo huo, ukienda kinyume kuna siku utapatwa na jambo kama msiba au sherehe jamii nzima inakususia inasema huyu hajui kuishi na watu[emoji849]