Nini maana ya kusamehe...?

...katika kosa linalouma ni kosa analoweza kukutendea spouse wako...
sasa nikiwapa mifano ya hayo makosa yasiyosameheka hapa mtasema
mbu anajipendelea...acha ni myuti nikiwasikiliza wengine wakimwaga sera hapa...

nitarudi baadae....

MBU 'spouse' wako ndo utegemee makosa makubwa zaidi..
why?
kwa sababu mmekutana ukubwani na kila mtu ana malezi yake
mimi nafikiri makosa makubwa ni ya ndugu wa damu ambao mmekuwa pamoja..
na ambao wanajua kabisa 'walilokufanyia' linauma kiasi gani..
lakini kwenye 'mapenzi' kuna visasi na kukomoana sometimes
usiposamehe unakuwa'umemfanya ashinde' kwa sababu
pengine aliazimia kukufanyia jambo 'la kukuumiza' milele..
na wewe kweli 'umekubali' kuumizwa milele...
 
Ni kweli kabisa Lizzy, kusamehe kuna leta hisia nzuri sana kwenye moyo wako na ofcoz Bosi kuwa ni 'afya'.
ukisamehe unajisikia mwepesi na 'comfortable' sana hata ukiwa na wale waliokutenda.
Usiposamehe unaumia sana.

Lakini tukumbuke pia kwamba kusamehe ni process jamani!
 
Mimi ninavyoelewa unapomsamehe mtu ina maana mnakuwa kama awali (hapa itategemea na situation). unaassume yale yote yalitokea hayakutokea.
Kwa mfano. Kama ni mke/mume alikucheat na ukaamua kumsamehe ina maana kwamba mtaendelea na maisha yenu kama kawaida.
Katika hali ya kibinadamu na kwa case kama hiyo wapo wanaoweza kusamehe na kuendelea kuishi pamoja na wapo ambao wanasamehe ila swala la kuishi pamoja ni gumu. Ni gumu kwasababu tunasamehe ila tunashindwa kusahau. Moyo huwa ni mzito sana kuvumilia maudhi na kuyasahau.
Kwa mfano nikikuuliza lizzy nitajie vipindi viwili ulivyokuwa na furaha....(hapa unaweza chukua muda kukumbuka). Nikikuuliza ni wakati gani ulikuwa na huzuni au ni mtu gani alikuletea huzuni nafikiri unaweza chukua sekunde kujibu.
Kuna watu huwa wanasema "katika maisha yangu sitokaa nisahau huyu desh desh alivyonitenda". Katika mazingira hayo unafikiri mtu wa namna hiyo anaweza kusamehe? Atasamehe vipi wakati moyo bado una chuki? Atasamehe vipi wakati ana tendency ya kukumbuka mabaya yanayomfika na kuyaweka kando mazuri?
Dah! Nimeandika sana, nitarudi b'dae.
 
Na mara nyingi watu wanashindwa kutoa msamaha kwasababu hiyo
Kufanyiwa kitu ambacho hukutarajia na mtu ambae hukutarajia kunafanya mambo yaonekane magumu zaidi.
Ni sawa na mtu kukutukana...mtu asiyekufahamu akifanya hivyo ni rahisi kupotezea tu maana huyo mtu hakujui..ila mtu unaetegemea akuheshimu na kukuongoza unapokosea akikuporomoshea matusi mtu unakua humiliated. Ila inabidi watu wajifunze kupita/shinda vitu kama hivyo.

Kwa kufanyiwa kitu ambacho hukustahili na mtu ambae hukuwahi kutegemea kitu kama hicho toka kwake fahamu kwamba ulimpandisha sana cheo (uli-over estimate mazuri yake) kisha umshushe mpaka pale anapostahili na kuamua kwamba halikua kosa lako kisha songa mbele.

...katika kosa linalouma ni kosa analoweza kukutendea spouse wako...
sasa nikiwapa mifano ya hayo makosa yasiyosameheka hapa mtasema
mbu anajipendelea...acha ni myuti nikiwasikiliza wengine wakimwaga sera hapa...

nitarudi baadae....

Hahhaha...Mbu bana hamna wakukusema..na akitokea SITOMSAMEHE..LOLZ!!
Unachoongelea kinaeleweka...sawa na hicho tunachojadili na Fynest.
Kwamba kuna kosa ambalo unaweza ukafanyiwa na watu hata kumi tofauti na kwa wote likawa na uzito tofauti kutokana na mahusiano yenu pia vile ulivyokua ukimchukulia huyo mwenzako.

Mwisho wa siku kumbuka kwamba kama bado ulichofanyiwa kinakusumbua hasara iko juu yako na aliyekutendea hana hata habari.
Samehe kwa faida binafsi...sio ya unaemsamehe.
....lol....haya bana...hahahha...
mchokozi sana wewe kumbe?...ngoja nijiulize...
can i trust you again?.....yes i can, but with caution!

haya, nawahi mahala...baadae


Hahahha...unalala na jicho moja wazi sio??
 
LIZZY!!

Mi nafikiri kuna kusamehe na kupuuzia, kupuuzia unasema tu kimoyomoyo issue niliotendewa sio issue ngoja niendelee na maisha yangu!! lakini kusamehe kunaenda na matendo, kama ulikua ni rafiki amsalimiani mnarudia na kama ni wapenzi mnarudiana provided tu sababu iliyowatenganisha imesemeheka na wote mkaridhia!!
 

... Hii afya inaitwa afya ya Utu!! ..Lol! tofauti na ile ya mwili.... Ni afya muhimu !
 

Boss hutakiwi kuishi na mtu huku ukitegemea the worst from them. It's not healthy...ukifikia hatua hiyo just call it a quit.
Spouse ...mpaka ukaamua kuishi na mtu na kumfanya partner wako maana yake umemwamini yeye na ndio ukamchagua yeye na sio mwingine. Ule ukaribu wenu (kushea nyumba..chakula..kitanda..hisia...watoto n.k ) ndivyo vinavyofanya utegemee kwamba atakutendea haki (kutokukudanganya..nyanyasa n.k.)...hivyo mtu ana kila haki ya kuumizwa sana na mtu ambae alimwamini hata kukubali kushirikiana nae kimaisha/kimwili na kuhisia.
 

Hus nimekusoma..
Ukiwa na chuki na mtu hujasamehe...
Kumsamehe kunaondoa hiyo chuki ila haina maana mapenzi yanarudi!!


Kwahiyo hata kama ni mwizi unajifanya kama vile sio mwizi kisa umemsamehe???
 


nafikiri point yangu ni sio 'kutegemea the worst'
bali kutokuwa 'suprised' yakitokea
 
Reactions: Mbu
Umenikumbusha ile unasema "Ahaaa fulani bana namuamini sana hawezi kunifanyia jambo lolote baya"
 
nafikiri point yangu ni sio 'kutegemea the worst'
bali kutokuwa 'suprised' yakitokea

Boss kutokua surprised maana yake uwe umejiandaa...kujiandaa maana yake uwe unategemea.
Huwezi kutokua surprised na kitu ambacho hukua umejiandaa nacho...na wala huwezi kujiandaa na kitu ambacho hukutegemea.
Vinafuatana!!
 
Aseeee!!
Duh!
sina kabisa 'culture' ya kupiga simu za chit chat
hata wale 'marafiki na ndugu'
nikipiga simu basi kuna kitu cha maana cha kuzungumza
sifanyi chit chat kwenye simu....
 
AJ hii ni nzuri nimeipenda...

... Afya ya namna hii (afya ya Utu)... tafiti zinaonesha inaogeza CD4 ... kuliko mboga mboga na matunda...Lol ..sio utani mkuu ni kweli chukulia na Mwenzio ..very close ..in day to day ..life ...lakini full of vinyongo, chuki, hasira..na hisia hasi nyingine... lazima ikate CD4... yaani Msamaha wa dhati ni dawa...ya Asili ..au? lol ...wala sio jambo la kujishauri ..Just do it!!
 
Boss kutokua surprised maana yake uwe umejiandaa...kujiandaa maana yake uwe unategemea.
Huwezi kutokua surprised na kitu ambacho hukua umejiandaa nacho...na wala huwezi kujiandaa na kitu ambacho hukutegemea.
Vinafuatana!!

aisee..
nahisi women wanavyo chukulia 'a relationship' ni tofauti na men...
kuna vitu mimi kama mimi huwa havinishangazi kabisa...
na hapo ni in general
sio specific kwa mtu fulani..
 
Hii ni ya utu, akili na mwili...lol
Ntarudi nikawsome kama mli conclude UTU ni nini!

Lolz .. Ilikuwa hkali ..kumbe ulipitia...hah hah..gaijin ..alitukimbia ..anakwenda kupima afya ya utu ..hakurudi ...

... Kumbe angetakiwa kupima ...AMESAMEHE...?
 
Reactions: bht

Kusamehe inamaanisha kutokumbuka ya nyuma.
Loading...
 
aisee..
nahisi women wanavyo chukulia 'a relationship' ni tofauti na men...
kuna vitu mimi kama mimi huwa havinishangazi kabisa...
na hapo ni in general
sio specific kwa mtu fulani..

This is not a gender issue Boss..
Ni namna watu wanavyochukulia na kuishi maisha!!
Kuna watu wanaishi kwa uangalifu...yeye anatembea barabarani huku akifikiria anaweza gongwa na gari...anakua na mpenzi akifikiria wanaweza achana wakati wowote and so so. Wengine wanachagua kufurahia maisha bila kufikiria mabaya yanayowezekana. Akiwa na mpenzi anaemwamini basi anaishia kwenye kumwamini bila kufikiria kwamba huyo mpenzi atavunja hiyo imani...sio kwamba hawajui uwezekano upo ila wanachagua kuucha uwe kwa wengine na kuamini kile alicho nacho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…