Mkoba wa Mama
JF-Expert Member
- May 5, 2021
- 208
- 91
Likizo inatoa nafasi kwa wanafunzi kupumzika na kujiandaa kwa muhula unaofuata, lakini pia inatoa nafasi kwa wanafunzi kukaa na familia na wazazi wao kwa pamoja. Lakini kuna baadhi ya shule wanazuia likizo za watoto na kuwaamuru waendelee kwenda shule kwa ajili ya kufundishwa.
Jambo la kushangaza hapa ni kwamba, mwaka wa masomo una jumla ya siku 194, sasa kama walimu wanashindwa kutumia vizuri huo mda kuwafundisha watoto? Itasaidia nini kuwazuia watoto kwenda likizo ya mwezi mmoja ili wawafundishe?
Wawaache watoto wakae likizo, wasiwachoshe, kama siku 194 hazitoshi kufundisha na kumaliza silabasi, basi watoe taarifa kwa wizara husika iongeze siku za masomo na ipunguze siku za likizo ili hilo nao lieleweke.
Kitu cha kushangaza zaidi, baadhi ya viongozi wa serikali ndio wanaamrisha jambo hili, hasa wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya, wakati wanafahamu kabisa utaratibu wa kalenda ya masomo kwa mwaka mzima.