lindunduru
JF-Expert Member
- Aug 2, 2015
- 392
- 553
nina pikipiki honda NX 650 Inatoa moshi mweusi wakati hard acceleration.nini sababu? Nini suluhu la hilo tatizo?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mosh mweusi hauna shida sana ila ungekuwa wa bluu au mweupe hapo ningekushauri cha kufanyaa ingawa hata huo mweusi ukizid sana itabidi wakuchekie rings .nina pikipiki honda NX 650 Inatoa moshi mweusi wakati hard acceleration.nini sababu? Nini suluhu la hilo tatizo?
Mafuta yanapoingia ndani ya injini (combustion chamber) hayawezi kuungua mpaka yawe yamechanganywa vizuri na hewa ya oxygen. Kiwango cha hewa kinachotakiwa kinategemea na ukubwa wa injini yenyewe. Sasa injini yoyote ya petroli inapotoa moshi mweusi ni dalili kuwa haichomi mafuta vizuri kwa sababu ya kuwepo kwa hewa pungufu kuliko mafuta. Kuna sehemu ya mafuta hutoka nje ya eksozi bila kuwa yameungua. Hakuna madhara makubwa kwa injini yako ila utakuwa unapoteza mafuta mengi bure na vile vile kudhuru mazingiria kwa sababu sehemu ya huo moshi mweusi ni Carbon Monoxide. Kuna sababu nyingi zinazoweza kusababisha hali hii itokee.nina pikipiki honda NX 650 Inatoa moshi mweusi wakati hard acceleration.nini sababu? Nini suluhu la hilo tatizo?
umeniponya hapo.nimebana jet tatizo limeisha.AsanteMafuta yanapoingia ndani ya injini (combustion chamber) hayawezi kuungua mpaka yawe yamechanganywa vizuri na hewa ya oxygen. Kiwango cha hewa kinachotakiwa kinategemea na ukubwa wa injini yenyewe. Sasa injini yoyote ya petroli inapotoa moshi mweusi ni dalili kuwa haichomi mafuta vizuri kwa sababu ya kuwepo kwa hewa pungufu kuliko mafuta. Kuna sehemu ya mafuta hutoka nje ya eksozi bila kuwa yameungua. Hakuna madhara makubwa kwa injini yako ila utakuwa unapoteza mafuta mengi bure na vile vile kudhuru mazingiria kwa sababu sehemu ya huo moshi mweusi ni Carbon Monoxide. Kuna sababu nyingi zinazoweza kusababisha hali hii itokee.
Kama Injini yako inatumia kabyureta, basi tafuta fundi akuchekia kabureta yako. Huwa kuna boya ambalo huenda sasa hivi lina kitundu kidogo kinachofanya boya lizame ndani ya mafuta na kusababisha kabyereta ishindwe kuzuia mafuta ya ziada na hivyo kuruhusu mafuta mengi yapite. Vile vile inawezekana jet inayopitisha mafuta imeshapanuka kupita kiasi. Kuna sababu nyingi sana zinazoweza kufanya kabureta isifanye kazi vizuri. Sababu nyingine huenda ni kwamba air fliter yako sasa hivi imeziba hairuhusu hewa ya kutosha kuingoia ndani ya injini.
Kama injini yako inatumia Electronic Fuel Injection (EFI) basi pia kuna sababu nyingi sana ingawa kubwa itakuwa ni kuwa ama Oxygen sensor yako imekufa au Air Filter imeziba au Injector nozzle zimepanuka hivyo zinahitaji kubadilishwa. Vile vile inawezekana engine control Unit yako imeharibika, ingawa hii ni nadra sana