Nini maana ya msemo "hujafa hujaumbika"

Nini maana ya msemo "hujafa hujaumbika"

Chochote kinaweza kukutokea ndani ya Kuishi kwako..!

Unaweza kuwa Kipofu au kiziwi au Kilema Chochote. Lakini Ukifa ndio inakuwa mwisho wa hadidhi yako hakutakuwa na mabadiliko zaidi.

Hujafa hujaumbika....!
 
Lolote baya linaweza kukuta muda wowote ukiwa hai.

Maana yake kuwa humble kesho its another day huwezijua
 
MTU aliyekufa ndo tayari ameumbika complete

Maana yake unapokuwa unaishi jambo lolote linaweza kuondoa ukamilifu wako.

Nakumbuka kuna watu walikuwa wanamcheka Lissu na kumuita CHIBA Ila Leo .......I can't go deep
 
Ni hadi pale mtu utapofariki ndio kuumbwa kwako kunakoma, kabla ya kifo uumbaji wako waendelea ndio maana mtu aweza zaliwa hana ulemavu lakini akaupata ulemavu ukubwani...

Ndio maana halisi ya hiyo methali...
 
Huu msemo na ule "kuwa uyaone" Kwasasa nailewa kuliko misemo yeyote Ile katika maisha kiufupi nimeiishi.
 
Leo unamiguu miwili utashangaa kesho huna,au umetobolewa macho au kuharibika kwa kiungo chochote kwa kuongezeka au kupungua....kile kitendo Cha kuwa na mwonekano mpya ndo msemo hutimia ....hujafa hujaumbika
 
Huu msemo wa Waswahili "hujafa hujaumbika" huwa una maana gani?
Mfano: kwa kuwa bakhresa bado anaishi inawezekana kabisa siku moja akakosa hata mia mbili ya kula mihogo
 
Hujaumbika hapo ina maana ya kukamilika Kwa umbo lako. ..so simple meaning hujafa hujakamilika. Unaweza pata ajali umbo likabadilika...
 
Hujafa hujaumbika: kuumbika (kuishi) hupelekea kufa (kupata changamoto na hatimaye umauti). Matatizo ndiyo yanamuumbua mwanadamu na kumwonesha jinsi alivyo hasa (duni, dhaifu, mnyonge, mwenye ukomo).
 
Kuumbika ni kuumbwa vizuri. Hivyo msemo huu unamaana kwamba ilimradi upo hai unawezapata madhira flani yakakubadili umbo au mwili wako.Vitu kama ajali, magonjwa nk.
 
Back
Top Bottom