Kujua maana ya nyongo mkalia ini inabidi ujue yafuatayo;
Nyongo au jina lingine bile, na ini au liver kwa lugha ya huko kwa malkia.
Nyongo na ini vipo pamoja katika mwili wa wanyama km binadamu,n.k na pia ndege kama kuku n.k
Kama ulishawahi kuchinja kuku au kuona ndani ya tumbo la kuku utaona nyongo ilivyo ndogo na imelalia na kukaa karibu sana na ini .
Sasa, maana ya msemo huo ni kuwa kwa wanaotumia maini kwa kula ni lazima wawe makini kuithamini nyongo vinginevyo itapasuka na kuingia kwenye ini na kumbuka maini ni matamu sana ila nyongo ni chungu sana.