Habari waungwana naomba msaada kwa mwenye kuelewa maana ya ndoto hii mara nyingi nimekuwa nikiota naendesha vyombo vya moto kama vile gari ya abiria au pikipiki huku nimepakia abiria nyuma.
Sometime naota narusha ndege angani yenye abiria wengi wakati huo sina experience yoyote na vyombo vya moto.
Hii ndoto inajirudia kwa miaka mingi sasa
Ndoto za safar ni ndoto zenye maana kubwa sana katika maisha yako kwa mtu aliye makini. Unaweza ukaota ndoto moja ikatasfr maisha yako yote mpaka unakufa.
Ukiota umeachwa na gai yaan ulkuwa stend alafa gar ikakuacha tafsiri yake ni ishara ya kukosa kazi au kuna jambo ulilotaka kulifanya basi ujue halitotimia. Ukiota umepanda gari iwe ya abiria au private na ukasafiri salama ni ishara ya ya kupata ulichokusudia na mambo yako yataenda sawiya.
Ukiota umeachwa na chombo chochota cha usafiri kwa kulala yaan ile mida imefika wewe umelala. Maana yake mafanikio yako yapo karibu ila huchangamki umebetekwa aidha kwa uvivu au kuna watu wanatembelea nyota yako. Ukiota umeachwa na usafiri ila kuna mtu kakuchelewesha aidha ki makusud bimaana muda wa kusafr anakupigisha stori ni ishara ya kuwa kuna mtu anakuchelewesha kwenye mafanikio yako yaweza ikawa mpenzi wako ndugu au jamaa zako.
Ukiota umeshapanda kwenye chombo cha usafri kisha ukashusha ikiwa sababu ni nauli bas ni ishara ya kuwa mbali na mungu. Ikiwa umeshusha kwa chuki na kwenye hilo gar wapo wachamungu viongozi wa dini ni ishara ya kuwa unaupenda na kuabudu sana uchawi na utakuchelewesha kwenye mambo yako.
Ukiota unaendesha gari ama pikipiki ni ishara ya mafanikio kupata ulichokusudia mipango yako kutimia. Ukiota upo safarkwa mguu kisha ukapewa lift ni ishara ya kusiadiwa utapata msaada lakini ni mara moja tu au upo shamba ghafla ukaona gar ni ishara pia kumaliza matatzo yako lakin pia kuna ishara ya msaada.
Ukiota unaendesha baiskeli ni ishara ya mafanikio yako yapo karibu lakini hakupasa utumie nguvu na uwe mvumilivu sababu baiskeli bila kunyonga kwa nguvu haiend. Ukiota umepandishwa kwenye baiskeli ni ishara ya shughuli unayoifanya au kazi itakucheleweshea mafanikio lakini utayapata ila kwa nguvu na uvumilivu.
Ukiota umepanda ndege ni ishara ya kuwa wewe ni mtu muhimu sana kwenye jamii yako na utakuwa juu kimafanikio. Ukiota upo ngani na usafiri usioeleweka aidha upo kwenye ungo au unasafiria kwa kuelea angani ni ishara ya kuchukulia kichawi kwenye safari zao.
Ukiota unaikimbiza gari ni ishara ya wewe kwamba una njama za kuzulumu siku za uson. Ukiota unakimbizwa na gari kwa speed kubwa na wewe unakimbia ishara ya mafanikio yako kuwa karibu lakini hujishughulish au pia kuna watu watakuwa wanakudhulumu ikiwa ni mchapa kazi.
Ukiota unasafirisha maiti na ukawapeleka sehem yenye mkusanyiko ni ishara ya kuuza kirahs unachouza au kupata kile ulichokusudia. Pia ukiota upo kwenye usafr na mpo na maiti ni ishara ya kuwa katika kazi au bishata zako kuna msaliti humo hayupo pamoja nawe.
Ukiota upo kwenye chombo chochote cha usafiri kisha ukapata ajali ni ishara ya kupata huzun na mawazo na kuna jambo litatokea kwako. Pia ukiota unawaona nduguzo wamepata ajali kuna huzun itatokea kwenye ukoo au familia yako. Pia ukiota upo kwenye chombo kibovubovu kikuukui yan chombo ambacho kina mashaka ya kusaifri ni ishara ya kuwa na haliduni katika maisha mambo yako kuzorota