Sijui nyota ni nini
Ila najua nyota yako ikiwaka siku moja tu kwenye maisha yako basi dunia nzima itakujua. (Mf Messi, Obama, Ronaldo, na wengine wengi)
Kila mtoto anazaliwa na nyota yake, lakini ili nyota ile ifikie malengo kuna jitihada binafsi za mzazi na mtoto na wanaomzunguka.
Huku Africa kuna uchawi wa kuiba, kuzika, kufifisha, kuifunika, kuichafua, na kuigawa nyota. Sijui kwingine.
Jukumu lako ni kujua nyota yako ni ipi (kila mtu ana yake ya tofauti )na ufanyeje ili ing'ae kupita za wengine.