haya maneno mawili nimekuwa nikiyasikia sana lakini sielewi maana yake msaada tafadhali.
Ndugu Katavi,
Kwa kuanzia: neno ombwe fafsiri yake ni "vacuum" kwa kugha ya kiingereza kama alivyosema mchangia mada mmoja hapo juu.
Na neno hilo, ombwe (vacuum), lina asili (kimatumizi) katika fizikia likimaanisha, kwa tafsiri rahisai sana, eneo ambalo lina mgandamizo mdogo sana wa hewa, hakuna hewa (gas or air) ya kutosha. Mathalani ipo kidogo sana kwa sababu ya mgandamizo wake kubanwa sana. (Mimi sio mtaalamu wa fizikia)
Katika siasa neno hili linatumika kama nahau isiyo rasmi (informally) katika msemo "ombwe la uongozi" i.e "leadership vacuum". Maana yake ni kuwa kuna ukosefu wa uongozi mahiri (au japo viongozi japo uongozi wao haukidhi viwango na matakwa-kwa maoni ya mzungumzaji). Ndio maana kila mambo ya uongozi wa nchi yetu yanapozidi kwenda mrama-hasa katika maamuzi wanasiasa, watu (hasa prof. Lipumba hapa Tz) husema "kuna ombwe la uongozi katika taifa letu"
Neno "WELEDI" au "ueledi" ni ile hali ya mtu kuwa mweledi yaani
mahiri katika jambo fulani. Unaweza pia kutumia neno "ubobevu" kumaanisha hali ya kubobea katika jambo fulani, mathalani taaluma. Kwa kiingereza ninaweza kulinganisha na "mastery of something" . He masters/is very conversant with the Swahili language = Ana ueledi /ubobevu katika lugha ya kiswahili.
Nadhani nimejaribu. Tuendelee kujifunza