Nini Maana ya "OMBWE" na "WELEDI"

Nini Maana ya "OMBWE" na "WELEDI"

Katavi

Platinum Member
Joined
Aug 31, 2009
Posts
42,023
Reaction score
12,811
haya maneno mawili nimekuwa nikiyasikia sana lakini sielewi maana yake msaada tafadhali.
 
'Ombwe' ni hali iliyopo nchini kwa sasa, hili neno lilikuwa halitumiki kwa sababu hali kama hii haikuwahi kuwepo hapo kabla!
 
'ombwe' ni hali iliyopo nchini kwa sasa, hili neno lilikuwa halitumiki kwa sababu hali kama hii haikuwahi kuwepo hapo kabla!
mkuu hapo umetuchanganya wengi, hali ya sasa ipii?? Yaani unamaanisha nini?
 
ombwe ni vacuum kwa kiingereza kama sikosei...weledi nadhani ni umahiri katika kufanya jambo fulani...ni mtazamo wangu huu...
 
majibu anayo Sangara ingawa hajiamini
 
majibu anayo Sangara ingawa hajiamini

mkuu si kwamba sijiamini...sina tafsiri iliyo rasmi ya maneno hayo ndio maana nikaweka kwa kifupi hivyo...naamini yanajitosheleza kwa kiwango chake.
 
Weledi nafikiri ni meritocracy - ufanyaji kitu kwa misingi ya merits that somebody has - people getting status/ rewards etc because of what they have attained, instead of their wealth or social status - kitu ambacho JK amekiua - anagawa vyeo km njugu ni si kwa misingi ya weledi.
 
Jamani wadau! Muulizaji kauliza kwa Kiswahili maana ya maneno ya Kiswahili kwa faida yake na wengine wengi kama mimi Mwendabure. Mbona mnatoa majibu ktk lugha mbili tofauti, Kiswahili na Kiingereza? Jitahidini naamini kiswahili mnakijua vema ila basi tu! Mnataka kutukoga wengine. Tuacheni mchezo ktk suala la Lugha yetu hii adhimu.
 
haya maneno mawili nimekuwa nikiyasikia sana lakini sielewi maana yake msaada tafadhali.

Ndugu Katavi,

Kwa kuanzia: neno ombwe fafsiri yake ni "vacuum" kwa kugha ya kiingereza kama alivyosema mchangia mada mmoja hapo juu.

Na neno hilo, ombwe (vacuum), lina asili (kimatumizi) katika fizikia likimaanisha, kwa tafsiri rahisai sana, eneo ambalo lina mgandamizo mdogo sana wa hewa, hakuna hewa (gas or air) ya kutosha. Mathalani ipo kidogo sana kwa sababu ya mgandamizo wake kubanwa sana. (Mimi sio mtaalamu wa fizikia)
Katika siasa neno hili linatumika kama nahau isiyo rasmi (informally) katika msemo "ombwe la uongozi" i.e "leadership vacuum". Maana yake ni kuwa kuna ukosefu wa uongozi mahiri (au japo viongozi japo uongozi wao haukidhi viwango na matakwa-kwa maoni ya mzungumzaji). Ndio maana kila mambo ya uongozi wa nchi yetu yanapozidi kwenda mrama-hasa katika maamuzi wanasiasa, watu (hasa prof. Lipumba hapa Tz) husema "kuna ombwe la uongozi katika taifa letu"

Neno "WELEDI" au "ueledi" ni ile hali ya mtu kuwa mweledi yaani mahiri katika jambo fulani. Unaweza pia kutumia neno "ubobevu" kumaanisha hali ya kubobea katika jambo fulani, mathalani taaluma. Kwa kiingereza ninaweza kulinganisha na "mastery of something" . He masters/is very conversant with the Swahili language = Ana ueledi /ubobevu katika lugha ya kiswahili.

Nadhani nimejaribu. Tuendelee kujifunza
 
OMBWE:
1. Uwazi katika kitu kilichotolewa hewa.
2. Mzunguko wa kisima unaozuia wateka maji wasiingie ndani ya kisima.

WELEDI:
Hali ya kuelewa na kufahamu kitu.
Wingi wa mweledi.

Chanzo (source) - Kamusi ya Kiswahili Sanifu, Toleo la Pili.
 
Ombwe ni utupu na weledi ni mbinu, ujuzi, stadi nk
 
Weledi nafikiri ni meritocracy - ufanyaji kitu kwa misingi ya merits that somebody has - people getting status/ rewards etc because of what they have attained, instead of their wealth or social status - kitu ambacho JK amekiua - anagawa vyeo km njugu ni si kwa misingi ya weledi.

kiswanglish ni msingi wa kuvuruga na kuharibu utamu wa lugha..mtu ameuliza maneno ya kiswahili anapewa majibu kwa kiingereza...mambo ya vipi haya GREAT THINKERS? kama hajui kiingereza inakuwaje? nashangaa???

tujifunze busara ya kuweka vitu pahala vinastahili...kama huna cha kuchangia ni bora kusoma kisha ukapita kuliko kupoteza nguvu na wakati kufanya yasiyostahili.
 
ombwe ni vacuum kwa kiingereza kama sikosei...weledi nadhani ni umahiri katika kufanya jambo fulani...ni mtazamo wangu huu...

Katika matumizi ya kila siku, ombwe(VACUUM) ni kiasi cha nafasi ya kuwa kimsingi ni tupu ya jambo , kwamba wake wa gesi shinikizo ni kidogo sana kuliko shinikizo anga .Wakati mwingine hujulikana kama "tupu". Utupu kamili itakuwa moja kwa chembe hakuna ndani yake kabisa, ambayo ni vigumu kufikia katika mazoezi. Fizikia mara nyingi kujadili matokeo ya mtihani bora ambayo ingeweza kutokea katika utupu kamilifu, ambayo wao tu kuwaita "vacuum" au "free nafasi", na kutumia neno sehemu ya utupu kwa kutaja utupu halisi.(source:wikiswahili)
 
Ombwe ni vacuum kama iliyosemwa na watangulizi.
Ueledi ni ufahamu wa jambo kwa uyakinifu na katika upembuzi wake. unaweza kuumithilisha na 'professionalism'
Pia ueledi ni namna ya kuliangalia jambo kwa jicho mujarabu
 
Ombwe maana yake utupu, uwazi na pengo na weledi ni wingi wa mweledi yaani muzi na stadi katika taaluma fulani. kwa mfano tunase,ma weledi wa masuala ya kisiasa na kadhalika. upo ndugu yangu?
 
Ombwe ni utupu wa kutokuwa na kitu kwa kipindi fulani, yawezekana mawazo, vitu au hali fulani. kwa mfano kwa sasa Tanzania ipo katika ombwe la maamuzi ya busara ndio maana inashindwa kuamua mambo yake muhimu mpaka yaamuliwe na nchi zingine...!
 
Ombwe maana yake utupu, uwazi na pengo na weledi ni wingi wa mweledi yaani muzi na stadi katika taaluma fulani. kwa mfano tunase,ma weledi wa masuala ya kisiasa na kadhalika. upo ndugu yangu?
Nimeelewa mkuu...
 
Back
Top Bottom