.. Juzi natoka kazini, getini nikakutana na mlinzi. (ni mzee hivi kdg ameniambia eti ni mnyantuzu japo kabila hili silijui). Katika kutambulishana maana mimi ni mgeni hapa ofisini nikamjuza jina langu na mkoa nitokapo..... Yaani Tanga.. Naye hakukawia kuniuliza.... Nini maana ya Tanga?... Nikajiumauma pale... Lakini sikumpa jibu sahihi... Hivi Nauliza... Tanga ina maana yoyote zaidi ya Tanga la msiba au tanga la jahazi?! Au tanga ni kutangatanga yaani kuhangahika?