Nini Maana ya "Tanga"?!

Nini Maana ya "Tanga"?!

Tanga ni neno LA KIBONDEI maana yake SHAMBA,,,, na pia kuna TANGA ile shuka ya Kuongoza JAHAZI..
 
Tanga maana yeke ni shamba,ni jina lililotokana na kabila moja pale jiji la wabondei,wakisema chaita tanga,wana maana ya twaenda shamba,

Pia tanga ni eneo linalopatikana karibu na bahari,hivyo ukisikia tanganyika maana yake ni eneo linalopatikana karibu na bahari na eneo lililoko mbali na bahari,jina ambalo lilianzishwa na wajerumani
 
Tanga inaweza maanisha lile shuka wanaloweka kwenye jahazi.

250px-Dhow_znz.jpg


Tanga pia inamaanisha kuzurura au kutembea sana au kutotulia sehemu moja, mfano mtu anaweza akasema bulshark kwa kutanga tanga tu hajambo, leo yupo jukwaa la michezo, kesho yupo jukwaa la siasa etc.

Tanga pia humaanisha nguo za ndani za kike, zina vikamba kama bikini lakini sio exactly bikini kwani nyuma zinakuwa pana kidogo.

Tanga pia humaanisha kundi la nyota.

source ya vingi wikipedia
Tanga - Wikipedia, kamusi elezo huru
Asante chief... Ila bullshark sitangitangi bhana.... Nipo JF tu..
 
maana yake ni "uvivu na uchawi uliokithiri" kama unabisha nenda tanga ukashuhudie mwenyewe
 
Wanyakyusa njooni hapa muwaambie wenzenu maana ya neno tanga(itanga)
 
Jina la tanga linatokana na kabila la kibondei wakimaanisha shamba... Watoto walipoulizwa na wazungu wazaziwenu wapo wapi wakajibu kwa kibondei waita ntanga.. Yani wameenda shamba wao wazungu wakakariri Tanga.. Kwamaelezo zaidi fika pale Urithi la makumbusho mkabala na magereza mkoa wa tanga.. Ahsante sana
 
Back
Top Bottom