Nini maana ya uchumi wa bluu?

Nini maana ya uchumi wa bluu?

Lastmost

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2022
Posts
802
Reaction score
919
Wakuu salaam.
Naomba kufahamishwa maana ya uchumi wa bluu.
Asanteni
 
Ni Uchumi ambao umejikita Kwenye vyanzo vyenye Rangi Ya Blue....!
Sijui 'Ushanfahamu hapo?
 
Umejibiwa Vema Hapo Juu
Lakini Wana Siasa Wao Wanazoa Tu Maneno Hata Kama Hayetekelezi
 
Ni Uchumi unaotokana na rasilimali za Bahari kama vile Mikoko na Matandawazi. Yaani imebeba dhana kuwa Blue Economy kutengeneza ajira pamona na kupambana au kuhimili mabadiliko ya tabianchi kupitia kulinda rasilimali zote za ukanda wa Pwani.
 
Bahari huonekana bluu.. ingawa maji yake sio bluu. Nchi inayopakana na bahari kama Zanzibar uchumi wake unategemea Utalii na shughuli za baharini kama uvuvi na mazao ya baharini kama mwani n.k wakaamua sasa wauvalie njuga uchumi kutokana na bahari.. uchumi wa bluu
 
Umejibiwa Vema Hapo Juu
Lakini Wana Siasa Wao Wanazoa Tu Maneno Hata Kama Ha

Umejibiwa Vema Hapo Juu
Lakini Wana Siasa Wao Wanazoa Tu Maneno Hata Kama Hayetekele

Ni Uchumi unaotokana na rasilimali za Bahari kama vile Mikoko na Matandawazi. Yaani imebeba dhana kuwa Blue Economy kutengeneza ajira pamona na kupambana au kuhimili mabadiliko ya tabianchi kupitia kulinda rasilimali zote za ukanda wa Pwani.
Asante mkuu,nimekusoma
 
Bahari huonekana bluu.. ingawa maji yake sio bluu. Nchi inayopakana na bahari kama Zanzibar uchumi wake unategemea Utalii na shughuli za baharini kama uvuvi na mazao ya baharini kama mwani n.k wakaamua sasa wauvalie njuga uchumi kutokana na bahari.. uchumi wa bluu
Shukrani mkuu, nimeelewa
 
Nadhani kuna nchi wanategema kwa kiasi kikubwa kukuza uchumi kupitia bahari na rasilimali zake. Ila kuna nchi hata wakitumia bado ni sehemu ndogo tu ya uchumi unakua. Kwa nchi kama Tanzania tukisema tunavuna kupitia uchumi wa bluu kiasi kwamba tutoboe huo ni urongo. .

Hata rasilimali za utalii peke yake haziwezi kutufanya kuwa uchumi mkubwa kwa sababu nchi kubwa duniani zinafaidika zaidi na viwanda na technology. Kuna cha kujifunza hapa. .
 
Lakini mkuu kwa Tanzania tatizo lipo kwenye allocation ya resources zetu na governance yetu haiko vizuri. Nadhani hata kwa rasilimali tulizonazo au sekta kama ya utalii pekee na blue economy zina uwezo wa kutunufaisha kabisa. Kwa sababu wenzetu wanafanya investment kwenye vuwanda na teknolojia maybe kutokana na strategic plans zao pia pengine hawana resources natural kama sisi hizi tuko nazo. Ila kiukweli ni sehemu au asilimia chache ya rasilimali zetu tukitumia vizuri tunapiga hatua.
 
ni pale unapoutofautisha na uchumi black, uchumi red, uchumi white, orange, violet etc ndo waweza ona uchumi wa blue
 
Uchumi wa Blue ni Uchumi wa kutegemea Rasilimali za baharini ambapo kutumia Bahari nchi inaamua kutumia chanzo hiko na kukiendeleza katika uchumi, uchumi wa blue umejikita katika Uvuvi wa kisasa, uchimbaji wa Mafuta baharini, tafiti mbalimbali, Usafirishaji, utengenezaji wa vyombo vya kusafiria nk... so ni Uchumi ambao unategemea kwa asilimia kubwa kuitumia bahari vizuri katika kuleta Maendeleo na mapinduzi katika uchumi.
 
Lakini mkuu kwa Tanzania tatizo lipo kwenye allocation ya resources zetu na governance yetu haiko vizuri. Nadhani hata kwa rasilimali tulizonazo au sekta kama ya utalii pekee na blue economy zina uwezo wa kutunufaisha kabisa. Kwa sababu wenzetu wanafanya investment kwenye vuwanda na teknolojia maybe kutokana na strategic plans zao pia pengine hawana resources natural kama sisi hizi tuko nazo. Ila kiukweli ni sehemu au asilimia chache ya rasilimali zetu tukitumia vizuri tunapiga hatua.

Point yangu ni kuwa tuangalie wenzetu nchi kubwa wamefanya nini kuletea nchi zao maendeleo, hicho ndio cha kujifunza. Kuna nchi kama Japani imezungukwa na bahari, na bado ina utalii kubwa kuliko Tanzania. Hawategemei tu utalii na rasilimali bahari, wamejikita sana kwenye viwanda na technologia kwa sababu ndio uelekeo wa dunia ya sasa. .

Ukitaka kufeli ni kuendekeza kutia nguvu kwenye mambo ambayo tulitakiwa kutia nguvu miaka 30 iliyopita. Kwa dunia ya sasa unakuta mtu anakwambia kilimo Kwanza, wakati hata nchi zinzolima bado zinapata faida kubwa na kilimo ni asilimia ndogo sana. Bado hatutaki kujifunza kwa wenzetu. .
 
Wajifya
 
Nadhani kuna nchi wanategema kwa kiasi kikubwa kukuza uchumi kupitia bahari na rasilimali zake. Ila kuna nchi hata wakitumia bado ni sehemu ndogo tu ya uchumi unakua. Kwa nchi kama Tanzania tukisema tunavuna kupitia uchumi wa bluu kiasi kwamba tutoboe huo ni urongo. .

Hata rasilimali za utalii peke yake haziwezi kutufanya kuwa uchumi mkubwa kwa sababu nchi kubwa duniani zinafaidika zaidi na viwanda na technology. Kuna cha kujifunza hapa. .
Zanzibar wanatumia Sana neno uchumi wa bluu,hivi ikatokea bara za zenj wakatengana kabisa, Zanzibar itatoboa kiuchumi?
Nasikia wazanzibar wengi hawaupendi muungamo
 
Uchumi wa Blue ni Uchumi wa kutegemea Rasilimali za baharini ambapo kutumia Bahari nchi inaamua kutumia chanzo hiko na kukiendeleza katika uchumi, uchumi wa blue umejikita katika Uvuvi wa kisasa, uchimbaji wa Mafuta baharini, tafiti mbalimbali, Usafirishaji, utengenezaji wa vyombo vya kusafiria nk... so ni Uchumi ambao unategemea kwa asilimia kubwa kuitumia bahari vizuri katika kuleta Maendeleo na mapinduzi katika uchumi.
Asante boss,maelezo murua
 
Zanzibar wanatumia Sana neno uchumi wa bluu,hivi ikatokea bara za zenj wakatengana kabisa, Zanzibar itatoboa kiuchumi?
Nasikia wazanzibar wengi hawaupendi muungamo
Unajua ubinafsi ni kitu kibaya sana na kikishakukaa basi tena. Wazee wetu walivyosema kuwa UMOJA ni Nguvu hawakukosea. Nakumbuka mwalimu wangu wa chuo wakati anatufundisha forms of business alinambia kuna tofauti kubwa kati ya Sole Proprietorship na Company au Patnership. Faida mojawapo ya company capitol wanayochanga inawatoa kuwa large scale business wakati mmoja mmoja anafanya proprietorship anakuwa small scale. Marekani kuungana kwao kumekuwa na faida kubwa sana hususani za kiuchumi. .

Kwa upande wa Zanzibar nadhani wanataka kuachana bila kutumia busara, kwa nin nasem hivi, naona Zanzibar wana manufaa makubwa tena kushinda sie tulivyo na manufaa nao; ardhi yao ndogo na wanahitaji ulinzi, umeme nk kutoka bara. Zanzibar ni sehemu ndogo sana ni mkoa kabisa, ila haiwezi kuwa yenyewe ikatoboa inavyofikiria, kwa kuzalisha karafuu au? Ukiangalia wanasema tuko nao kwa sababu za kiusalama, yani Zanzibar ndo itulinde sie au? Ila hata ikitoka bado itahitaji kuwa chini ya mtu mwingine tu kama sio mwarabu sijui. .
 
Back
Top Bottom