Nini madhara ya chanjo?

Nini madhara ya chanjo?

Slave

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2010
Posts
5,313
Reaction score
2,646
Kuna watu wengi nimewaona ambao ni vilema mguu mmoja wengi wao wanasema kilema walikipata wakiwa wadogo baada ya kuchomwa sindano za chanjo,je kwanini inakwa hivyo?
 
Salam, hilo suali ni tata kidogo ila ntajaribi kulijibu kwa uzoefu, maana sijui hiyo sindano ya chanjo alichomwa wapi, kwa mana chanjo kuna za matone Mdomoni, na zilobaki mara nyingi ni mkononi au pajani, hivyo kuathirika mguu moja kwa moja hadi kusababisha ulemavu si rahisi.
Lakini kama itatokea kuchomwa sindano ya **** hapo inawezekana kupata ulemavu kama mchomaji atamchoma sindano ambayo kwa bahati mbaya au kutokujua atauchoma na mshipa wa fahamu (sciatic nerve) ambao husambaza hisia sehemu ya mguu athari yake ni kupooza kwa mguu huo (paralisis) na mgonjwa huuburuza mguu huo, hata hivyo kwa vile sindano ni nyembamba mara nyingi mhusika anaweza kupona baada ya mda wa kutumia baadhi ya dawa na kufanyiwa mazoezi ya kitaalam (physiotherapy).
Uzoefu unaonesha kwenye miaka ya 70-80 watoto wengi waliathirika na polio (kupooza) lakini kabla dalili za kupooza kujitokeza hupata homa na hapo huambiwa wakapate chanjo lakini inakuwa too late chanjo kufanya kazi na ndipo husema wameathirika na chanjo kumbe ni kinyume chake.
Karibu tena
 
Back
Top Bottom