Nilikuwa mtumiaji wa kuberi zilipopigwa stop nikahamia kwenye ugoro, nakumbuka nikiwa 1st yr chuo jamaa angu wa Tanga alinifundisha kutumia ugoro. Stim lake Ni balaa, nikazoea had tukajuana watumiaji hostel mzima, mtu anakuja kukugongea mlango saa7 usiku. Tulifahamiana karibia wote.
Nilikuwa addicted had naanza kazi sikuweza kuacha, nilipooa nilikuwa nauficha bafuni au popote pale ambapo naweza kuingia na kuutumia bila wife kujua, lakini alinikamata nao. Ugoro ni utumwa. Mikono ilikuwa inatetemeka Sana na mdomon kuwa na vidonda.
Sasa Nina zaidi ya miaka 7 sijatumia, ila rafiki angu aliyenifundisha hajaweza kuacha, me nakunywa mvinyo yeye Bado anakula ugoro alafu Ni Headmaster Sasa na amekiri kushindwa kuacha.
Ugoro Ni hatari, Bora beeeer na konyagi aisee.