Nini maoni yako kuhusu video assistant Referees?

Haki kweli inapunguza mchecheto wa ushangiliaji. Though inaleta usawa pale madhambi yanapotokea. Yaan badala ya mtu mwingine kuonewa. Sijui nini kifanyike
 
Hii nimeipenda kulikuwa na udanganyifu mwingi sana katika mabao ya kuotea. Wanaosema imepunguza msisimko ni vigeugeu maana timu yake ikifungwa goli la offside mpaka matusi ya nguoni yanamtoka lakini wakifunga la offside wanasema inaondoa msisimko.
 
Ni ujinga mkubwa wa teknolojia hiyo yaani inaboa mfano ureno peoe alifunga goli wakashangilia, zaid ya sek 40 wanasubiri majibu afu unaambiwa sio goli yaan inakera sana mpira ni mbinu ili ushinde game
 
me naiona ya kiboya tu.. kma jana Chile wamefunga goli refa kakataa bdae tena kakubali inakua kma game ya yanga na mbeya city
 
Baada ya miaka kadhaa itakuwa sawa tu, ubongo wa mwanadamu huwa unahitaji kuzoea jambo jipya kabla ya kuliafiki...

Miaka mingi iliyopita mchezo wa mpira wa miguu haukuwa na offside, na pale sheria hiyo ilipoanzishwa kulikuwa na malalamiko mengi maana ilionekana ya ajabu lakini ilitumika na inaendelea kutumika (Nadhani ndio sheria iliyofanyiwa mabadiliko mengi na imekuwa ikiwasumbua sana waamuzi)

Sisi wengine tuliozoea kutazama na kufuatilia michezo kadhaa kama mpira wa kikapu, mpira wa wavu, riadha, tenis n.k tumeshazoea kuona mchezo ukisimama na mwamuzi kujiridhisha kwa kutazama marudio mgando ya picha...
 
Visingizio kwa waafrika sasa ndo vinaisha

tnasingiziaga sana marefa
sasa hii teknolojia inapaswa kutufanya tuache kulia lia
Kuna msisimko fulani pale nyavu zinapotingishwa huu utaratibu unauondoa.
 
Kikubwa waboreshe tu, refa asiwe uwanjani awe kati ya hao wenye video ili msisimko ubaki pale pale kama mwanzo.
 
Inaboa kinoma yani ikitiwa kwenye ligi ntajipanga kuwa mfuatiliaji wa muvi za kihindi tu
 
Tutaizoea taratibu ndugu zangu wapenda soccer.. Hii technology inatumika pia kwenye NBA na msisimko umebaki palepale.. Cha msingi ni kuondokana na uonevu na maumuzi tata ndani ya pitch!!!!
Hongereni sana FIFA.
 
Naiunga mkono hii technology kwa asilimia zote, haya ni mapungufu madogo madogo ambayo marefaa nina uhakika watayafanyia marekebisho.

Mwanzoni wakati inaingizwa kwenye mchezo wa Rugby pia kulikua na malalamiko chungu nzima lakini yakafanyiwa marekebisho saiz tuna enjoy tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…